Monday, December 21, 2015

WAISLAMU WAWAOKOA WAKRISTO KUTOKA MIKONONI MWA ALSHABAB

Watu wawili wameuwawa na wengine watatu kujeruhiwa vibaya baada ya wapiganaji wa kundi la al Shabaab kushambulia basi moja la abiria lilokuwa likielekea eneo la Mandera Kaskazini mwa kenya kutoka Nairobi.
Shambulio hilo la kigaidi lilitekelezwa hii leo asubuhi.
Walioshuhudia wameambia mwandishi wa BBC kuwa abiria wa kiislamu waliwalinda wenzao wakristo kwa kukataa kugawanywa kwa makundi.
Wasafiri waislamu nchini Kenya walilazimika kuingilia kati kuokoa maisha ya wakristu waliokuwa nao katika basi lililotekwa na wapiganaji wa Alshabaab.
Waislamu hao walitahamaki walipotekwa na wapiganaji wa Al Shabaab kisha wakaanza kutenganishwa katika makundi mawili ya waislamu na wasio waislamu.
Hapo ndipo waligundua nia yao ni kuwaua kama walivyofanya katika mauaji kama hayo mwaka uliopita.
Mhudumu wa kampuni ya basi la Makkah ameithibitishia BBC tukio hilo katika barabara ya kutoka Mandera kuelekea mjini Nairobi.
Mwezi Novemba mwaka uliopita wapiganaji wa Al Shabaab waliteka basi moja na kuwaua abiria 28 ambao hawakuwa Waislamu.
Kundi hilo liligonga vichwa vya habari mwezi Aprili lilipowaua wanafunzi wakristo 148 katika chuo kikuu cha Garissa.

HISTORIA YA KRISMASI

JUA HISTORIA YA SIKUKUU KUBWA YA CHRISTMAS NA SHAMLASHAMLA ZAKE Kwa muda mrefu sikukuu ya krismasi imejulikana kuwa na sikukuu kubwa sana na inaweza kuwa ya kwanza kusherehekewa na watu wengi duniani na dini karibu zote. sikukuu hii ambayo hukumbuka kuzaliwa kwa Yesu kristo hapa duniani. katika nchi zilizoendelea huwa wanaanza shamla shamla za sikuu hii tangu mwezi wa November maduka nyuma ofisi hupambwa na kuanza kuuza vitu vyingi vinavyohusiana na sikukuu hii kubwa Duniani. kumekuwa na utata wa mambo mengi ikiwa uhusika wa father Chrismas, miti ya michrismas pamoja na taa za vimweku mavazi mekundu na meupe. nataka leo tuangalie uhusika wa baba christmas mwenye ndevu nyeupe rangi ya uwaridi mashavuni na anavaa nguo nyekundu.hii imetokana na tangazo la biashara lililobuniwa na kampuni moja ya vinywaji baridihuko america ya kasikazini kati ya mwaka 1931. katika miaka ya 1950 baathi ya watu huko brazil walijaribu kubadili cheo cha baba chrismass na kumpa mtu wa taifa lao waliyemwita babu wa India. matokeo yalikuwaje? si kuwa tu babu chrismas alimshida babu wa India bali imeendelea kutumika kama nembo kubwa ya kibiashara kupita hata wale wanaoadhimisha kuzaliwa kwa Yesu.  
Historia ya kuanza kwa sikukuu ya Chrismasi
 
Katika karne 2 za mwanzo tangu kuzaliwa kwa Yesu, hapo ulipoaanza ukristo, watu wengi hawakuserehekea siku za kuzaliwa wala kufa kwa wafia imani au hata ya Yesu mwenyewe. kinasema Encyclopedia Britannica kwa nini? wakristo waliona kusherehekea siku ya kuzaliwa ni mazoea ya kipagani linalopaswa kuepukwa, licha ya msimamo wa wakristo wa nyakati hizo ya kupinga mazoea ya kusheherekea siku ya kuzaliwa, kanisa katoriki ndilo lilianza kusheherekea chrismas katika karne ya nne. kipindi hicho kanisa lilitaka kujiimalisha na kupunguza umaarufu wa sikuu za dini za kipagani za roma ambazo zilikuwa zinafanyika katika msimu wa baridi, jua linapokuwa upande wa kasikazini wa Dunia kila mwaka, kuanzia December 17 mpaka Januali 1. Waroma wengi walisherehekea pamoja walicheza, walishiriki katika matamasha, magwaride, na sherehe nyingine walizokuwa wakiabudu miiungu yao, kitabu cha chrismas America kilichoandikwa na Penne L. Restand kinasema ilipofika December 25 waroma walisherehekea kuzaliwa kwa jua lisiloweza kushindwa. hivyo ilibidi kanisa kuwa na ushawishi mkubwa wa kuwashawishi waroma kugeuza siku hiyo ya kuzaliwa jua iwe ni siku ya kuzaliwa Yesu, na ilifanyika ili kuuondoa ibada za kipagani ijapo waroma waliweza kufurahia vitu vyote au michezo yote waliokuwa wakifanya katika msimu wa baridi. kitabu cha Santa Claus, a Biography kilichoandikwa na Gerry Bowler kwa hakika waroma waliendelea kusherehekea hiyo sikuu mpya kama walivyo zoea kufanya zamani. Biblia Inasema Nini Kuhusu Krismasi? Biblia haitaji tarehe ambayo Yesu alizaliwa, wala haisemi kwamba tusherehekee siku yake ya kuzaliwa. Kama vile kitabu McClintock and Strong’s Cyclopedia kinavyosema: “Mwadhimisho wa Krismasi haukuagizwa na Mungu, wala hautokani na AG [Agano Jipya].”Kinyume cha hilo, historia ya Krismasi inafunua kwamba inatokana na sherehe za kipagani.. Historia ya desturi za Krismasi Kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Yesu: “Wakristo wa karne ya kwanza hawakusherehekea siku ya kuzaliwa kwa [Yesu] kwa sababu waliiona sherehe ya kuzaliwa kwa mtu yeyote kuwa desturi ya wapagani.”—The World Book Encyclopedia. Desemba 25: Hakuna uthibitisho wowote kwamba Yesu alizaliwa tarehe hiyo. Huenda viongozi wa Kanisa walichagua tarehe hiyo ili ipatane na sherehe za kipagani zilizofanywa wakati wa au karibu na majira ya baridi kali. Kupeana zawadi, sherehe, karamu: Kitabu The Encyclopedia Americana kinasema: “Desturi nyingi za kujifurahisha zinazofuatwa wakati wa Krismasi zinatokana na Saturnalia, sherehe ya Waroma iliyofanywa katikati ya mwezi wa Desemba. Kwa mfano, karamu zenye madoido mengi, kupeana zawadi, na kuwasha mishumaa zilitokana na sherehe hii.” Kitabu Encyclopædia Britannica kinasema kwamba “hakuna kazi wala biashara iliyofanywa” wakati wa Saturnalia. Taa za Krismasi: Kitabu The Encyclopedia of Religion kinasema kwamba wazungu walirembesha nyumba zao kwa “taa na mimea ya kijani-kibichi ya kila aina” ili kusherehekea majira ya baridi kali na ili kuwazuia roho waovu. Mlimbo, mholi: Kwa kawaida mimea hiyo hutumiwa kama mapambo wakati wa Krismasi. “Wadruidi (makasisi Waselti) walisema kwamba mlimbo ulikuwa na nguvu za kimuujiza. Mholi, mmea ambao haunyauki, uliabudiwa kama ahadi ya kurudi kwa jua.”—The Encyclopedia Americana. Mti wa Krismasi: “Kuabudu miti lilikuwa jambo la kawaida kati ya wapagani wa Ulaya na waliendelea na zoea hilo baada ya kuwa Wakristo.” Kati ya mazoea yaliyobaki ya ibada hiyo ya miti ni desturi ya “kuweka mti wa Krismasi kwenye mwingilio au ndani ya nyumba wakati wa sikukuu zinazofanywa katikati ya majira ya baridi kali.”—Encyclopædia Britannica. 
Hiyo ndiyo historia ya chrismasi na vitu vyake vyote na siku za leo imekuwa ni siku ya kibiashara zaidi na kupeanza zawadi na ndo maana ikaanzishwa na boxing day yani siku ya kufungua mabox ya zawadi watu walizopeana wakati wa Christmasi. Blog tunakutakia wewe msomaji wetu Merry Christmas na heri ya mwaka mpya wa 2016.

USHUHUDA;NILINYOLEWA NYWELE ZOTE SEHEMU ZA SIRI NA WACHAWI USIKU NIKIWA NIMELALA


Naitwa Prisca mwenyeji wa mkoa wa Arusha napenda nishuhudie kitu ambacho kimetokea maishani mwangu hadi kupelekea kuokoka. mwaka 2010 kwa sababu ya kutafuta maisha nilikwenda zanzibar kuishi huko na nilipata chumba cha kupangwa maeneo ya airport na niliishi vizuri tu na majirani ambao tulikua tumepanga pamoja na kama binadamu ukiwa bado unayapenda ya dunia na shetani ametawala maisha yako niliamua kuwa na mpenzi mwanajeshi na uhusiano wetu uliendelea kwa muda kidogo. Baada kama ya miezi 6 nilianza kupatwa na matatizo mara niugue ghafla na nikienda kupima naambiwa sina ugonjwa wowote na hadi nilienda kwa mganga wa kienyeji maeneo ya unguja ukuu lakini ndio kwanza matatizo yaliongezeka. Baada kama ya mwezi mmoja baadaye vituko viliongezeka maana siku moja nilikuta nywele upande mmoja wa kichwa zimenyolewa zote ukweli nililia sana na kusema MUNGU mbona haya yananipata mimi? siku mbili baadae nikiwa natoka kazini maana nilikua hotelia nilikuta watu wananiongea mimi na nilijificha ili nisikie kile wanasema niliwasikia wakisema ''HILI LI DADA NI LI KICHWA NGUMU SANA YAANI LICHA YA KULITUMIA MAJINI YAKALILALA NA LICHA YA KULINYOA NYWELE KICHWANI BADO TU HALITAKI KUMWACHIA HUYU MWANAUME AMBAYE AMETUKATAA SISI WENYEJI NA KULIKUBALI HILI JINGA SASA HUYU MWANAUME ATA-SHARE MAPENZI NA MAJINI YETU HADI ATAMCHUKIA '' nilishtuka sana na kuanza kulia na baada ya muda nilisikia mmoja akisema ''LEO NDIO FINAL NA BAADA YA LEO ATAMWACHA TU HUYU MWANAUME'' nilishindwa kujizuia na kutokea na kuwambia mbona kunitesa hivyo je kosa langu ni nini? walicheka sana na dada mmoja kati yao akaniambia kama najipenda niachane na Sam ambaye ndiye mpenzi wangu na tulikua tumepanga kuoana kabisa niliingia ndani na kuanza kulia na jioni hiyo Sam alikuja na kunikuta nalia lakini nilimdanganya kuwa tumbo linauma ndio maana nalia na yeye kunisaidia na baadaye alienda kazini jioni hiyohiyo. siku hiyo nilisema silali ili nione kitakachoendelea na hata sijui nini kilitokea maana nilijikua nimeshalala na niliamka asubuhi na kukuta sehemu zangu za siri zimechafuka na pia kubwa kuliko yote na ambalo limesababisha kuandika haya ni kuwa nywele zote za sehemu yangu ya siri zilikua zimenyolewa na wembe nililia na kujiuliza maswali mengi sana yasiyo na majibu kwamba hivi inawezekana kweli mtu ukanyolewa nywele zote za sehemu ile bila kujijua? . Asubuhi waliendelea kunicheka na kusema walichobakiza ni kuniua. Nilikaa bila amani kwa zaidi ya wiki tangu siku hiyo huku kila siku nikisikia vitisho usiku kila siku mara kelele,miabga ya ajabu ajabu,na vitisho vingi mwisho nikakata tamaa ya kuishi na siku moja nikawaza kama ni kufa ngoja nikafie kanisani japokuwa mimi nilikua mpagani. Kesho yake baada ya siku hiyo nilienda kanisani la kilokole na kukuta vijana na watoto kama 7 wakiimba kwaya niliwauliza mchungaji yuko wapi wakaniambia mchungaji wao yuko safarini Dar nilichukia sana na mkubwa wa wale vijana akanikaribisha kukaa na kusikiliza nyimbo nikamwambia nina shida na mchungaji na nataka aniombee kwani nina matatizo makubwa na nakalibia kufa yule kijana alinitazama na kuniuliza kwamba '' UNAAMINI KWAM,BA YESU KRISTO ANAWEZA KUKUPONYA?'' nilikubali akaniambia nipige magoti na wao wataniombea kiukweli nilikataa maana nilijua labda mchungaji pekee ndio anaweza kuniombea na si waoa ambao wote nawazidi umri hata kama yule kaka kiongozi ni kama namzidi miaka 3 naye ni mwanajeshi. Kaka yule alinisihi sana na kuniambia sio mchungaji anayeponya bali anayeponya ni MUNGU na wao watamwomba MUNGU na mimi nitapokea uponyaji. Nilikataa na kusema nitakuja siku mchungaji akirudi lakini moyo unakataa na kusema naweza kufa kabla mchungaji kuja mikakubali lakini kwa masharti kwamba aniwekee mkono yule kiongozi wao tu na sio wale watoto yule kaka akaniambia ni mwamini MUNGU wanayemwabudu kwani hakuna linaloshindikana kwa JEHOVAH na akaniambia kwamba nitashuhudia kanisani kile ambacho MUNGU atatenda kupitia watoto hao kweli nilikubali kuombewa na wakaniombea nikapoteza fahamu na baada ya muda nikazinduka nikiwa nimepona yule kijana akaniambia kwamba nilikua na mapepo mengi sana lakini YESU amenifungua na kweli nilijihisi mwepesi na niko tofauti sana na nilivyokuja na wakaniwekea mikono tena kuniombea ulinzi wa MUNGU na baada ya hapo wakaniambia sitachezewa tena na wachawi labda tu nimwache huyu YESU aliyeniponya . Niliwaahidi kwamba sitamwacha YESU na nitamshawishi mchumba wangu naye aokoke. Nilirudi nyumbani hakuna aliyeniongelesha na yule dada nilimkuta analia na kusema nimemkomesha kwani majini yake yote 51 yamekufa. sikusema kitu na nikaingia ndani na kumshukuru sana MUNGU hata kama nilikua sijajua kuomba lakini kwa maneno machache niliomba. Tangu muda huo sikupatwa na tatizo lolote na niliishi kwa furaha na niliamua kumweleza yote mchumba wangu akashangaa na akakubali kuokoka hivyo tangu feb 2011 akaokoka na baadae tukaoana na hadi sasa tuko ndani ya YESU. sina la kusema ila namshukuru sana BWANA YESU kwa kuniponya na kuniokoa na hadi sasa niko salala sifa na utukufu ni kwa MUNGU BABA wa mbinguni. AMEN. picha hii haihusiani na Prisca lakini inaonyesha jinsi BWANA YESU anavyotenda miujiza kwa kuponya mangoja na nkufungua kila kifungo cha adui kilichokuwa kimefunga watu

MAAGIZO YA MUNGU Na Mtumishi Peter Mabula.


BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Kushika maagizo ya MUNGU ni jambo la muhimu sana. Malaki 3:7 ''Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema BWANA wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani?'' ''Mmegeuka mkayaacha maagizo yangu asema BWANA'' Kuna wanadamu wengi waliogeuka na kuyaacha maagizo ya MUNGU. Neno ''maagizo'' maana yake ni maelekezo yatolewayo na mkuu kwa anayemuongoza. Neno ''Maelekezo'' ni muongozo wa kufanya jambo. Maagizo ya MUNGU ni muongozo wa MUNGU uliotolewa na MUNGU kwa ajili ya wanadamu wote kuishi kwa kufuata muongozo huo. Muongozo wa MUNGU ambao wanadamu wote wanatakiwa kuufuata ni mmoja tu yaani Biblia takatifu. Zaburi 112:1 ''Haleluya. Heri mtu yule amchaye BWANA, Apendezwaye sana na maagizo yake.'' Kila agizo la MUNGU juu ya maisha ya kila mtu liko katika Biblia takatifu ambalo ni Neno hai la MUNGU kwa watu wote. Katika Biblia utapata muongozo wa jinsi ya kuishi ukimpendeza MUNGU na wanadamu. Kutokufuata Neno la MUNGU ambalo ndilo muongozo ni kumdharau MUNGU aliyeutoa. Yeremia 47:7a ''Utawezaje kutulia, Ikiwa BWANA amekupa agizo? '' Kuna maagizo mengi ya MUNGU kwetu. =Agizo la kwanza nikuokoka kwa kumpokea YESU kama Mwokozi wako. Yohana 3:16-19 ''Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. '' =Agizo la pili ni Kutubu dhambi zote. Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.-Mathayo 3:2 =Agizo la tatu ni kuacha dhambi zote na kuanza kutenda mema yanayoagizwa na Biblia. Zaburi 34:14 '' Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie.'' =Agizo la nne ni uwe mtakatifu siku zote. 1 Petro 1:14-16 '' Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. '' Kuna madhara makubwa sana kwa mtu anayeenda kinyume na maelekezo ya MUNGU. Maelekezo ya MUNGU ni wanadamu waishi maisha ya Wokovu ambao maisha hayo yako pekee katika KRISTO YESU. =Kumkataa YESU KRISTO ni kumkataa MUNGU. =Kuukataa Wokovu wa BWANA YESU ni kuukataa uzima wa milele. Kila mtu amehubiriwa injili lakini sio wote waliitii injili ya KRISTO japokuwa waiijua kwenye fahamu zao kwamba injili hiyo ndio muongozo pekee wa uzima wa milele kwao. Biblia inasema hivi huwa kuna wakati wa MUNGU kuwaacha waasi ili wafuate wanachokiamini kilicho nje na Wokovu wa KRISTO lakini mwisho ni hukumu ya kutisha. Warumi 1:21-25 ''Kwa Sababu, Walipomjua MUNGU Hawakumtukuza Kama Ndiye MUNGU Wala Kumshukuru; Bali Walipotelea Katika Uzushi Wao, Na Mioyo Yao Yenye Ujinga Ikatiwa Giza. Wakijinena Kuwa Wenye Hekima Walipumbazika; Wakaubadili Utukufu Wa MUNGU Asiye Na Uharibifu Kwa Mfano Wa Sura Ya Binadamu Aliye Na Uharibifu, Na Ya Ndege Na Ya Wanyama, Na Vitambaavyo. Kwa Ajili Ya Hayo MUNGU Aliwaacha Katika Tamaa Za Mioyo Yao, Waufuate Uchafu Wao, Hata Wakavunjiana Heshima Miili Yao. Kwa Maana Waliibadili Kweli Ya MUNGU Kuwa Uongo, Wakakisujudia Kiumbe Na Kukiabudu Badala Ya MUUMBA Anayehimidiwa Milele, Amina'' Kuna watu hupotoshwa na viongozi wao wa dini. Kiongozi akianguka dhambini ni rahisi kuwaangusha waumini. Kuna ambao wameangushwa na viongozi wao wakuu wa kikanisa ngazi ya dunia. Kama askofu mkuu wa kanisa lenu ataanguka ni rahisi pia maaskofu wadogo kuanguka. Ni rahisi kwa wachungaji kuanguka. Ni rahisi zaidi kwa waumini kuanguka na kuiacha kweli ya KRISTO. Ndugu Yangu, Ni Hatari Mtu Akufundishe Uongo Na Wewe Unasema "amina Kubwa". -Ni Hatari Mtu Akuhubiri Maagizo Yake Wewe Uyashike Huku Mmeacha Maagizo Ya MUNGU. -Ni Hatari Kwako Uliyemjua JEHOVAH MUNGU Wa Kweli Ambaye Anapatikana Katika KRISTO YESU Pekee, Lakini Kwa Tamaa Ya Pesa Au Kushawishiwa Umeamua Kumwacha. -Ni Hatari Kwako Unayesujudia Sanamu Za Wanadamu Au Wanyama Na Kuziabudu. BWANA YESU Kwa Sauti Kali Anasema Geuka. ''Msigeuke kuandama sanamu, wala msijifanyizie miungu ya kusubu mimi ndimi BWANA, MUNGU wenu-Walawi 19:4'' Mwenye sikio la kusikia na kuacha mabaya na asikie leo. Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka. Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu. Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo. Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu. MUNGU wangu akubariki sana na akupe ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako. ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo yangu. Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula. 0714252292. mabula1986@gmail.com Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili

VIKAO VYA UOVU Na: DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP AMOS KOMBA (RP),

Utangulizi wa Somo: Uovu ni mambo yoyote mabaya yanayotendwa na yanayofanywa na watu waovu. Ikumbukwe kuwa 'Waovu ni Watu'. Anaweza akawa mtu yoyote yule awe ndugu, mama au baba. Hawa watu wanaufanya uovu na siku haiishi bila kufanya uovu. Furaha ya muovu inaonekana pale anapofanya uovu wake!!. Imeandikwa katika METHALI 2:14-15… [Wafurahio kutenda mabaya; Wapendezwao na upotoe wa waovu; 15 Waliopotoka katika njia zao; Walio wakaidi katika mapito yao.]…kwani Mungu aliwaumba watu ili wafanye uovu? Jibu ni hapana. Ila kwa sababu ya hila za watu, kupotoka kwa watu na tamaa za watu wakaamua kumtafuta mfamle wa uovu wakaungana naye ili wafanye uovu. Imeandikwa katika YEREMIA 5:26… [Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu..]… Imeandikwa pia katika 1TIMOTHEO 5:15….[Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani.].. Kinachosababisha ni tamaa za watu na chuki za watu. Watu wengine huwa wanaamua waende kanisani wakisema ‘nikatafute kiti nikae kanisani, niandae Bibilia yangu nimsikilize mchungaji nitoke nitakuwa sawa’… Hiyo ni sawa lakini si sawa sana…Lakini wakati wanaposoma neno na kulitafakari ndipo watakaa sawa. Ni jukumu la kila mtu kuwa na bidii ya kusikiliza mahubiri kwa bidii na kuyatafakari. Kwenye hili, jitihada ya kuingia ndani ya neno ni ya kila mtu. Kumbe sio lengo la Mungu kuwaumba watu ili wawe waovu, watu walipokuja duniani ila kwa hila zao, tamaa zao na chuki zao wakaaamua waungane na mfalme wa uovu ili waufanye uovu Kabla ya kutuma uovu wanaanza kwanza kujadili uovu huu utakuwa upi na nani watakaoupeleka na namna ya kuupeleka wanakotaka uende. Lazima wanafahamu kwanza huyo mtu Watu hawa wanaweza wakawa ni ndugu zako, wakati mwingine wanaweza wasiwe ndugu wa karibu, kama haajamfahamu huyu mtu wanatuma wapelelezi, wajue unachofanya kila wakati, baada ya hapo wanarudisha taarifa kwenye vikao vyake, wakati wa bidii, wakati wa kuchoka na kila maneno wanayooongea, kwa hiyo wakishafahamu wanaamua kutuma saa ukiwa na udhaifu. UKIRI Baba Mungu katika jina la Yesu kama kuna wapelelezi wametumwa kwenye maisha yangu nawakataa kwa jina la Yesu. Kwa jina la Yesu ikiwa kuna wapepelezi wametumwa kutokea katika vikao vya waovu nawasambaratisha kwa jina la Yesu. Amen Imeandikwa katika injili ya Luka kwamba kulikuwa na wapelelezi waliokuwa wanamviziavizia Yesu. Nakataa kwa jina la mtu yeyeyote anayenivizia anayenipekeleza ili anijue mchana huu wa leo nakataa kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazarethi. Hawa wapelelezi hawaleti tukio ila wanatafuta kukujua. Baada ya hapo wanarudi kwenye kikao chao wanatoa taarifa. Mfano Musa aliwatuma wapelelezi kwenye nchi ile ni nchi ya namna gani, watu wa namna gani, wanapigana je n.k. Kati ya hao kulikuwa na makundi mawili ambayo walirudisha majibu kwa namna ya rohoni na namna ya mwilini. Hata wapelelezi wanachaguliwa wenye akili ya kuona mbali, nani ana uwezo wa kugeuka akaja kwako kama rafiki, au mtu wa karibu… wana akili sana. Na hawa wapelelezi wanaotumwa huwa wanalipwa. Mfano pepo unaweza ukaliambia toka likakataa kwa sababu limeahidiwa malipo baada ya kazi hiyo. Hawa Wapelelezi wanatafuta kukufahamu. Mfano Hamani alikuwa na shida na Mordekai hivyo Hamani akatafuta watu akawalipa ili wampekeleze Mordekai. Immeandikwa katika ESTA3:1-5..[Baada ya hayo mfalme Ahasuero alimwongezea cheo Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, akampandisha, akamwekea kiti chake juu ya maakida wote waliokuwapo pamoja naye. 2 Nao watumishi wote wa mfalme, walioketi mlangoni pa mfalme, wakainama na kumsujudia Hamani, maana ndivyo alivyoamuru mfalme kwa habari zake. Bali Mordekai hakuinama, wala kumsujudia. 3 Basi watumishi wa mfalme walioketi mlangoni pa mfalme wakamwambia Mordekai, Mbona wewe waihalifu amri ya mfalme? 4 Ikawa, waliposema naye kila siku asiwasikilize, wakamwarifu Hamani, ili kuona kama mambo yake Mordekai yatasimama; maana alikuwa amewaambia ya kuwa yeye ni Myahudi. 5 Hata Hamani alipoona ya kwamba Mordekai hainami wala kumsujudia, alighadhibika sana.]… Kumbuka Hata shetani alitaka Yesu amuainamie. Hamani alipelekewa taarifa kuwa Mordekai huwa hainami kila anapopita. Hamani akajaribu kupita wote waliinama lakini Mordekai hakuinama na Hamani akajua kuwa huyu Mordekai hayupo peke yake. Wana wa Israel wametolewa Misri wanapekwa Kaanani wapetishwa jangwani nguo walizovaa hazikuisha wala kuchafuka wala viatu. Mungu huyu ni wa ajabu. Hamani aliamua ili ainamiwe vizuri alimua na kupanga kuwaangamiza Wayahudi pamoja na Mordekai. Alifanya haya yote kwa sababu ya wivu na kupenda sifa. Kumbuka kuwa anayesimamisha mambo siyo Mordekai bali anayesimamisha mambo ni aliye nyuma ya Mordekai (Mzee wa siku.) Wapo wale walioesema “tuone kama ataolewa”, “kama biashara yake itaendelea”, “kama atamaliza chuo” n.k….. Kumbbuka kuwa kuona wataona lakini hawatapata. Ni kweli utaona lakini sio yale unayoyawaza; ila utaona kivingine.. ESTA 3:5-13…[ 5 Hata Hamani alipoona ya kwamba Mordekai hainami wala kumsujudia, alighadhibika sana. 6 Akaona si shani kumtia mikono Mordekai peke yake; maana wamemjulisha kabila yake Mordekai; kwa hiyo Hamani alitaka kuwaangamiza Wayahudi wote waliokuwa wakikaa katika ufalme wote mzima wa Ahasuero, yaani, watu wake Mordekai. 7 Basi mwezi wa kwanza, ndio mwezi wa Nisani, mwaka wa kumi na mbili wa mfalme Ahasuero, wakapiga Puri, yaani kura, mbele yake Hamani; siku kwa siku, na mwezi kwa mwezi, hata mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari. 8 Basi Hamani akamwambia mfalme Ahasuero, Kuna taifa moja waliotawanyika na kukaa mahali mahali katikati ya mataifa walioko katika majimbo yote ya ufalme wako. Nao sheria zao zimefarakana na sheria za kila taifa; wala hawazishiki amri za mfalme; kwa hiyo haimpasi mfalme kuchukuliana nao. 9 Basi, mfalme akiona vema, na iandikwe kwamba waangamizwe; nami nitalipa talanta kumi elfu za fedha mikononi mwao watakaosimamia shughuli hiyo, waziweke katika hazina ya mfalme. 10 Ndipo mfalme alipoivua pete yake mkononi, akampa Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi. 11 Kisha mfalme akamwambia Hamani, Hiyo fedha umepewa, na watu pia, fanya uonavyo vema. 12 Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza; na barua zikaandikwa, kama vile Hamani alivyoagiza vyote, kwa maakida wa mfalme, na maliwali waliokuwa juu ya kila jimbo, na wakuu wa kila taifa; kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; zikaandikwa kwa jinsi la mfalme Ahasuero, na kutiwa muhuri kwa pete yake. 13 Barua zikapelekwa kwa mikono ya matarishi mpaka majimbo yote ya mfalme kuwaangamiza Wayahudi wote, na kuwaua, na kuwafisha, vijana kwa wazee, watoto wachanga na wanawake pia, siku moja, yaani, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili ndio mwezi wa Adari; na kuyachukua mali yao kuwa nyara.]… Hawa wapelelezi huwa wanalipwa. Unaona Hamani alikuwa tayari kulipa watakaochaguliwa na mfamle Ahusuero kuwangamiza Wayuhudi… Sio kila mtu huwa anakuwa katika vikao vya uovu…ila anachagua walio karibu na mkeo. Je Una mke bingwa wa kutoa mawazo.? Je yote huwa uanayafanyia kazi? UKIRI Kwa jina la Yesu ninaugeza mauovu waliyoyachilia kwangu urudi kwao walioutuma. Marafiki waliokusanya kwa ajili yangu wakakaa ili kuniharibia kikao hicho nakisambaratisha kwa Jina la Yesu. Amen Tunapoungumzia vikao kuna vikao vya aina mbili vya kiroho na kimwili. UKIRI Kwa mamlaka ya jina la Yesu nasambaratisha vikao vyote vya uovu kwa jina la Yesu na yote yaliopangwa yawapate wao. Kwa jina la yesu kila aliye kaa kwenye kikao mabaya yote ywapate wao kwa jina la YESU. Amen
Na: DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP AMOS KOMBA (RP), UFUFUO NA UZIMA. Utangulizi wa Somo: Uovu ni mambo yoyote mabaya yanayotendwa na yanayofanywa na watu waovu. Ikumbukwe kuwa 'Waovu ni Watu'. Anaweza akawa mtu yoyote yule awe ndugu, mama au baba. Hawa watu wanaufanya uovu na siku haiishi bila kufanya uovu. Furaha ya muovu inaonekana pale anapofanya uovu wake!!. Imeandikwa katika METHALI 2:14-15… [Wafurahio kutenda mabaya; Wapendezwao na upotoe wa waovu; 15 Waliopotoka katika njia zao; Walio wakaidi katika mapito yao.]…kwani Mungu aliwaumba watu ili wafanye uovu? Jibu ni hapana. Ila kwa sababu ya hila za watu, kupotoka kwa watu na tamaa za watu wakaamua kumtafuta mfamle wa uovu wakaungana naye ili wafanye uovu. Imeandikwa katika YEREMIA 5:26… [Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu..]… Imeandikwa pia katika 1TIMOTHEO 5:15….[Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani.].. Kinachosababisha ni tamaa za watu na chuki za watu. Watu wengine huwa wanaamua waende kanisani wakisema ‘nikatafute kiti nikae kanisani, niandae Bibilia yangu nimsikilize mchungaji nitoke nitakuwa sawa’… Hiyo ni sawa lakini si sawa sana…Lakini wakati wanaposoma neno na kulitafakari ndipo watakaa sawa. Ni jukumu la kila mtu kuwa na bidii ya kusikiliza mahubiri kwa bidii na kuyatafakari. Kwenye hili, jitihada ya kuingia ndani ya neno ni ya kila mtu. Kumbe sio lengo la Mungu kuwaumba watu ili wawe waovu, watu walipokuja duniani ila kwa hila zao, tamaa zao na chuki zao wakaaamua waungane na mfalme wa uovu ili waufanye uovu Kabla ya kutuma uovu wanaanza kwanza kujadili uovu huu utakuwa upi na nani watakaoupeleka na namna ya kuupeleka wanakotaka uende. Lazima wanafahamu kwanza huyo mtu Watu hawa wanaweza wakawa ni ndugu zako, wakati mwingine wanaweza wasiwe ndugu wa karibu, kama haajamfahamu huyu mtu wanatuma wapelelezi, wajue unachofanya kila wakati, baada ya hapo wanarudisha taarifa kwenye vikao vyake, wakati wa bidii, wakati wa kuchoka na kila maneno wanayooongea, kwa hiyo wakishafahamu wanaamua kutuma saa ukiwa na udhaifu. UKIRI Baba Mungu katika jina la Yesu kama kuna wapelelezi wametumwa kwenye maisha yangu nawakataa kwa jina la Yesu. Kwa jina la Yesu ikiwa kuna wapepelezi wametumwa kutokea katika vikao vya waovu nawasambaratisha kwa jina la Yesu. Amen Imeandikwa katika injili ya Luka kwamba kulikuwa na wapelelezi waliokuwa wanamviziavizia Yesu. Nakataa kwa jina la mtu yeyeyote anayenivizia anayenipekeleza ili anijue mchana huu wa leo nakataa kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazarethi. Hawa wapelelezi hawaleti tukio ila wanatafuta kukujua. Baada ya hapo wanarudi kwenye kikao chao wanatoa taarifa. Mfano Musa aliwatuma wapelelezi kwenye nchi ile ni nchi ya namna gani, watu wa namna gani, wanapigana je n.k. Kati ya hao kulikuwa na makundi mawili ambayo walirudisha majibu kwa namna ya rohoni na namna ya mwilini. Hata wapelelezi wanachaguliwa wenye akili ya kuona mbali, nani ana uwezo wa kugeuka akaja kwako kama rafiki, au mtu wa karibu… wana akili sana. Na hawa wapelelezi wanaotumwa huwa wanalipwa. Mfano pepo unaweza ukaliambia toka likakataa kwa sababu limeahidiwa malipo baada ya kazi hiyo. Hawa Wapelelezi wanatafuta kukufahamu. Mfano Hamani alikuwa na shida na Mordekai hivyo Hamani akatafuta watu akawalipa ili wampekeleze Mordekai. Immeandikwa katika ESTA3:1-5..[Baada ya hayo mfalme Ahasuero alimwongezea cheo Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, akampandisha, akamwekea kiti chake juu ya maakida wote waliokuwapo pamoja naye. 2 Nao watumishi wote wa mfalme, walioketi mlangoni pa mfalme, wakainama na kumsujudia Hamani, maana ndivyo alivyoamuru mfalme kwa habari zake. Bali Mordekai hakuinama, wala kumsujudia. 3 Basi watumishi wa mfalme walioketi mlangoni pa mfalme wakamwambia Mordekai, Mbona wewe waihalifu amri ya mfalme? 4 Ikawa, waliposema naye kila siku asiwasikilize, wakamwarifu Hamani, ili kuona kama mambo yake Mordekai yatasimama; maana alikuwa amewaambia ya kuwa yeye ni Myahudi. 5 Hata Hamani alipoona ya kwamba Mordekai hainami wala kumsujudia, alighadhibika sana.]… Kumbuka Hata shetani alitaka Yesu amuainamie. Hamani alipelekewa taarifa kuwa Mordekai huwa hainami kila anapopita. Hamani akajaribu kupita wote waliinama lakini Mordekai hakuinama na Hamani akajua kuwa huyu Mordekai hayupo peke yake. Wana wa Israel wametolewa Misri wanapekwa Kaanani wapetishwa jangwani nguo walizovaa hazikuisha wala kuchafuka wala viatu. Mungu huyu ni wa ajabu. Hamani aliamua ili ainamiwe vizuri alimua na kupanga kuwaangamiza Wayahudi pamoja na Mordekai. Alifanya haya yote kwa sababu ya wivu na kupenda sifa. Kumbuka kuwa anayesimamisha mambo siyo Mordekai bali anayesimamisha mambo ni aliye nyuma ya Mordekai (Mzee wa siku.) Wapo wale walioesema “tuone kama ataolewa”, “kama biashara yake itaendelea”, “kama atamaliza chuo” n.k….. Kumbbuka kuwa kuona wataona lakini hawatapata. Ni kweli utaona lakini sio yale unayoyawaza; ila utaona kivingine.. ESTA 3:5-13…[ 5 Hata Hamani alipoona ya kwamba Mordekai hainami wala kumsujudia, alighadhibika sana. 6 Akaona si shani kumtia mikono Mordekai peke yake; maana wamemjulisha kabila yake Mordekai; kwa hiyo Hamani alitaka kuwaangamiza Wayahudi wote waliokuwa wakikaa katika ufalme wote mzima wa Ahasuero, yaani, watu wake Mordekai. 7 Basi mwezi wa kwanza, ndio mwezi wa Nisani, mwaka wa kumi na mbili wa mfalme Ahasuero, wakapiga Puri, yaani kura, mbele yake Hamani; siku kwa siku, na mwezi kwa mwezi, hata mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari. 8 Basi Hamani akamwambia mfalme Ahasuero, Kuna taifa moja waliotawanyika na kukaa mahali mahali katikati ya mataifa walioko katika majimbo yote ya ufalme wako. Nao sheria zao zimefarakana na sheria za kila taifa; wala hawazishiki amri za mfalme; kwa hiyo haimpasi mfalme kuchukuliana nao. 9 Basi, mfalme akiona vema, na iandikwe kwamba waangamizwe; nami nitalipa talanta kumi elfu za fedha mikononi mwao watakaosimamia shughuli hiyo, waziweke katika hazina ya mfalme. 10 Ndipo mfalme alipoivua pete yake mkononi, akampa Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi. 11 Kisha mfalme akamwambia Hamani, Hiyo fedha umepewa, na watu pia, fanya uonavyo vema. 12 Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza; na barua zikaandikwa, kama vile Hamani alivyoagiza vyote, kwa maakida wa mfalme, na maliwali waliokuwa juu ya kila jimbo, na wakuu wa kila taifa; kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; zikaandikwa kwa jinsi la mfalme Ahasuero, na kutiwa muhuri kwa pete yake. 13 Barua zikapelekwa kwa mikono ya matarishi mpaka majimbo yote ya mfalme kuwaangamiza Wayahudi wote, na kuwaua, na kuwafisha, vijana kwa wazee, watoto wachanga na wanawake pia, siku moja, yaani, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili ndio mwezi wa Adari; na kuyachukua mali yao kuwa nyara.]… Hawa wapelelezi huwa wanalipwa. Unaona Hamani alikuwa tayari kulipa watakaochaguliwa na mfamle Ahusuero kuwangamiza Wayuhudi… Sio kila mtu huwa anakuwa katika vikao vya uovu…ila anachagua walio karibu na mkeo. Je Una mke bingwa wa kutoa mawazo.? Je yote huwa uanayafanyia kazi? UKIRI Kwa jina la Yesu ninaugeza mauovu waliyoyachilia kwangu urudi kwao walioutuma. Marafiki waliokusanya kwa ajili yangu wakakaa ili kuniharibia kikao hicho nakisambaratisha kwa Jina la Yesu. Amen Tunapoungumzia vikao kuna vikao vya aina mbili vya kiroho na kimwili. UKIRI Kwa mamlaka ya jina la Yesu nasambaratisha vikao vyote vya uovu kwa jina la Yesu na yote yaliopangwa yawapate wao. Kwa jina la yesu kila aliye kaa kwenye kikao mabaya yote ywapate wao kwa jina la YESU. Amen

Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu

JINSI YA KUDAI HAKI YAKO MBELE ZA MUNGU NA MTUMISHI WA MUNGU PETER M. MABULA



BWANA YESU asifiwe ndugu yangu. Nakukaribisha tujifunze jinsi ya kudai haki zetu mbele za MUNGU. Tunajua tunadai haki kwa nani? Haki zetu tunazidai pale ambapo tunauhitaji wa jambo Fulani mbele za MUNGU. Ni lazima tumjue vyema tunayemdai. Je tunasifa za kudai hicho tunachotaka? Isaya 54:17 (Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA. ) Watu wengi hatujui jinsi ya kudai haki zetu mbele za MUNGU, Watu wengi hatufahamu tudai nini, Watu wengi hua tunajaribu tu kudai lakini hatuna imani ya kupokea na wengine hatujampokea BWANA YESU ambaye ndio chanzo cha haki yetu yote hivyo hatuwezi kupokea. Kuna haki zinafahamika zinafahamika na kuna haki hatuzijui. Muda mwingi unawaza ‘’hivi MUNGU hanioni?’’ Wakati mwingine unawaza ‘’Mbona Fulani kafanikiwa?’’ Yeremia 1:19 ( Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema BWANA, ili nikuokoe. ) Tatizo sio kujua ila tatizo ni kutambua haki yako mbele za MUNGU. Tujikubali kwa maneno na kwa matendo pia. Haki ya MUNGU haionekani kwa macho hadi pale haki yako itakapofanya kazi ndio utaona matokeo mazuri. Kutoka 15:1-18(Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia BWANA wimbo huu wakanena, na kusema, Nitamwimbia BWANA, kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini. BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni MUNGU wangu, nami nitamsifu; Ni MUNGU wa baba yangu, nami nitamtukuza. BWANA ni mtu wa vita, BWANA ndilo jina lake. Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa baharini, Maakida yake wateule wamezama katika bahari ya Shamu. Vilindi vimewafunikiza, Walizama vilindini kama jiwe. BWANA, mkono wako wa kuume umepata fahari ya uwezo, BWANA, mkono wako wa kuume wawaseta-seta adui. Kwa wingi wa ukuu wako wawaangusha chini wanaokuondokea, Wapeleka hasira yako, nayo huwateketeza kama mabua makavu. Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa, Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa chungu, Vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari. Adui akasema, Nitafuatia, nitapata, nitagawanya nyara, Nafsi yangu itashibishwa na wao; Nitaufuta upanga wangu, mkono wangu utawaangamiza. Ulivuma kwa upepo wako, bahari ikawafunikiza; Wakazama kama risasi ndani ya maji makuu. Ee BWANA, katika miungu ni nani aliye kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu? Ulinyosha mkono wako wa kuume, Nchi ikawameza. Wewe kwa rehema zako umewaongoza watu uliowakomboa, Kwa uweza wako uliwaelekeza hata makao yako matakatifu. Kabila za watu wamesikia, wanatetemeka, Wakaao Ufilisti utungu umewashika. Ndipo majumbe wa Edomu wakashangaa, Watu wa Moabu wenye nguvu tetemeko limewapata, Watu wote wakaao Kanaani wameyeyuka. Hofu na woga umewaangukia; Kwa uweza wa mkono wako wanakaa kimya kama jiwe; Hata watakapovuka watu wako, Ee BWANA, Hata watakapovuka watu wako uliowanunua. Utawaingiza, na kuwapanda katika mlima wa urithi wako, Mahali pale ulipojifanyia, Ee BWANA, ili upakae, Pale patakatifu ulipopaweka imara, BWANA, kwa mikono yako. BWANA atatawala milele na milele. ). -Maandiko hapo juu yanaonyesha Musa na wana wa Israeli walitambua haki yako mbele za MUNGU . -Hapo juu inaonyesha kwamba huwezi kumsifu mtu usiyemuona. -Itambue haki yak oleo kwa MUNGU. -BWANA amkekupa haki tena, unaweza kuomba lolote kwake ukapata. -Usijisahau kwamba wewe ni mwenye haki, Palilia haki yako mbele za MUNGU siku zote. BWANA YESU asifiwe. Usikubali kulea tatizo ndani ya moyo wako. Usilidharau tatizo lako kwamba ni dogo sana bali shughulika nalo hata kama ni dogo sana. Ndugu yangu uliyekombolewa kwa damu ya YESU KRISTO, Baada ya kukombloewa ulitakaswa na kupewa haki ya MUNGU katika KRISTO. Lakini wateule wengi wana UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIROHO. -Haki yako idai huku ukiwa na sababu kabisa kwamba haki yako ni halali kwako. -Watu wengi huona tu vinavyoonekana lakini visivyoonekana ni vibaya zaidi, visivyoonekana ni mambo mabaya unayokusudia moyoni mwako. Isaya 43:25-26 (Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako. Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako. ). Je unaijua kesho yako katika MUNGU ikoje? Mambo mengine tunapanga sisi lakini tambua kwamba mengine MUNGU ndiye anapanga, lakini MUNGU hakuwazii mabaya hata siku moja bali yeye anakuwazia mema tu. Yeremia 29:11( Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. ). Palilia maisha yako ya kiroho. Palilia safari yako ya mbinguni. Mfuate ROHO wa MUNGU siku zote za maisha yako. Luka 18:1(Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba MUNGU sikuzote, wala wasikate tamaa. ) Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana . Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula Maisha ya Ushindi Ministry. 0714252292