JUA HISTORIA YA SIKUKUU KUBWA YA
CHRISTMAS NA SHAMLASHAMLA ZAKE Kwa muda mrefu sikukuu ya krismasi imejulikana
kuwa na sikukuu kubwa sana na inaweza kuwa ya kwanza kusherehekewa na watu
wengi duniani na dini karibu zote. sikukuu hii ambayo hukumbuka kuzaliwa kwa
Yesu kristo hapa duniani. katika nchi zilizoendelea huwa wanaanza shamla shamla
za sikuu hii tangu mwezi wa November maduka nyuma ofisi hupambwa na kuanza
kuuza vitu vyingi vinavyohusiana na sikukuu hii kubwa Duniani. kumekuwa na
utata wa mambo mengi ikiwa uhusika wa father Chrismas, miti ya michrismas
pamoja na taa za vimweku mavazi mekundu na meupe. nataka leo tuangalie uhusika
wa baba christmas mwenye ndevu nyeupe rangi ya uwaridi mashavuni na anavaa nguo
nyekundu.hii imetokana na tangazo la biashara lililobuniwa na kampuni moja ya
vinywaji baridihuko america ya kasikazini kati ya mwaka 1931. katika miaka ya
1950 baathi ya watu huko brazil walijaribu kubadili cheo cha baba chrismass na
kumpa mtu wa taifa lao waliyemwita babu wa India. matokeo yalikuwaje? si kuwa
tu babu chrismas alimshida babu wa
India bali imeendelea kutumika kama nembo
kubwa ya kibiashara kupita hata wale wanaoadhimisha kuzaliwa kwa Yesu.

Historia
ya kuanza kwa sikukuu ya Chrismasi

Katika karne 2 za mwanzo tangu kuzaliwa kwa
Yesu, hapo ulipoaanza ukristo, watu wengi hawakuserehekea siku za kuzaliwa wala
kufa kwa wafia imani au hata ya Yesu mwenyewe. kinasema Encyclopedia Britannica
kwa nini? wakristo waliona kusherehekea siku ya kuzaliwa ni mazoea ya kipagani
linalopaswa kuepukwa, licha ya msimamo wa wakristo wa nyakati hizo ya kupinga
mazoea ya kusheherekea siku ya kuzaliwa, kanisa katoriki ndilo lilianza
kusheherekea chrismas katika karne ya nne. kipindi hicho kanisa lilitaka
kujiimalisha na kupunguza umaarufu wa sikuu za dini za kipagani za roma ambazo
zilikuwa zinafanyika katika msimu wa baridi, jua linapokuwa upande wa
kasikazini wa Dunia kila mwaka, kuanzia December 17 mpaka Januali 1. Waroma
wengi walisherehekea pamoja walicheza, walishiriki katika matamasha, magwaride,
na sherehe nyingine walizokuwa wakiabudu miiungu yao, kitabu cha chrismas
America kilichoandikwa na Penne L. Restand kinasema ilipofika December 25
waroma walisherehekea kuzaliwa kwa jua lisiloweza kushindwa. hivyo ilibidi
kanisa kuwa na ushawishi mkubwa wa kuwashawishi waroma kugeuza siku hiyo ya
kuzaliwa jua iwe ni siku ya kuzaliwa Yesu, na ilifanyika ili kuuondoa ibada za
kipagani ijapo waroma waliweza kufurahia vitu vyote au michezo yote waliokuwa
wakifanya katika msimu wa baridi. kitabu cha Santa Claus, a Biography
kilichoandikwa na Gerry Bowler kwa hakika waroma waliendelea kusherehekea hiyo
sikuu mpya kama walivyo zoea kufanya zamani. Biblia Inasema Nini Kuhusu
Krismasi? Biblia haitaji tarehe ambayo Yesu alizaliwa, wala haisemi kwamba
tusherehekee siku yake ya kuzaliwa. Kama vile kitabu McClintock and Strong’s
Cyclopedia kinavyosema: “Mwadhimisho wa Krismasi haukuagizwa na Mungu, wala
hautokani na AG [Agano Jipya].”Kinyume cha hilo, historia ya Krismasi inafunua
kwamba inatokana na sherehe za kipagani.. Historia ya desturi za Krismasi
Kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Yesu: “Wakristo wa karne ya kwanza
hawakusherehekea siku ya kuzaliwa kwa [Yesu] kwa sababu waliiona sherehe ya
kuzaliwa kwa mtu yeyote kuwa desturi ya wapagani.”—The World Book Encyclopedia.
Desemba 25: Hakuna uthibitisho wowote kwamba Yesu alizaliwa tarehe hiyo. Huenda
viongozi wa Kanisa walichagua tarehe hiyo ili ipatane na sherehe za kipagani
zilizofanywa wakati wa au karibu na majira ya baridi kali. Kupeana zawadi,
sherehe, karamu: Kitabu The Encyclopedia Americana kinasema: “Desturi nyingi za
kujifurahisha zinazofuatwa wakati wa Krismasi zinatokana na Saturnalia, sherehe
ya Waroma iliyofanywa katikati ya mwezi wa Desemba. Kwa mfano, karamu zenye
madoido mengi, kupeana zawadi, na kuwasha mishumaa zilitokana na sherehe hii.”
Kitabu Encyclopædia Britannica kinasema kwamba “hakuna kazi wala biashara
iliyofanywa” wakati wa Saturnalia. Taa za Krismasi: Kitabu The Encyclopedia of
Religion kinasema kwamba wazungu walirembesha nyumba zao kwa “taa na mimea ya
kijani-kibichi ya kila aina” ili kusherehekea majira ya baridi kali na ili
kuwazuia roho waovu. Mlimbo, mholi: Kwa kawaida mimea hiyo hutumiwa kama
mapambo wakati wa Krismasi. “Wadruidi (makasisi Waselti) walisema kwamba mlimbo
ulikuwa na nguvu za kimuujiza. Mholi, mmea ambao haunyauki, uliabudiwa kama
ahadi ya kurudi kwa jua.”—The Encyclopedia Americana. Mti wa Krismasi: “Kuabudu
miti lilikuwa jambo la kawaida kati ya wapagani wa Ulaya na waliendelea na zoea
hilo baada ya kuwa Wakristo.” Kati ya mazoea yaliyobaki ya ibada hiyo ya miti
ni desturi ya “kuweka mti wa Krismasi kwenye mwingilio au ndani ya nyumba
wakati wa sikukuu zinazofanywa katikati ya majira ya baridi kali.”—Encyclopædia
Britannica.

No comments:
Post a Comment