Utangulizi wa Somo: matukio ya Kichawi
ni matukio yanayotokea kufuatana na uchawi kuhusishwa. Duniani leo, zipo nguvu
nyingi za giza zinazotumiwa na wanadamu, na nguvu hizo ni UCHAWI. Malengo ya
wachawi au wanadamu kutumia uchawi ni: · Kuwaumiza watu wengine kimazingara ·
Watu wengine hutumia uchawi ili kujilinda · Wengine tu huutumia uchawi kwa
ajili ya kujifurahisha. Hawa ni wale ambao wakiwatesa watu wengine hufurahia
kuona mateso yale. Yesu alisema, “furaha yangu ni kuona mapeznzi ya Baba yangu
yanatimia”. Upande wa shetani wao hufurahi kuona mabaya yakitokea. · Wengine
hutumia uchawi kwa ajili ya kufanya miujiza /mazingaumbwe n.k. Imeandikwa
katika HESABU 23:23…[Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu
ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani
aliyoyatenda Mungu!]…. Inamaanisha kuwa, endapo uchawi haupo, basi mtu anaweza
kufanya jambo nalo likafanikiwa. Wachawi huwa na mawasiliano ya karibu na roho
za mashetani. Katika Biblia wapo amaboa waliwahi kutengenezewa matukio: Mfano
1: MATHAYO 9:32-34…[Hata hao walipokuwa wakitoka, tazama, walimletea mtu bubu
mwenye pepo. 33 Na pepo alipotolewa, yule bubu alinena, makutano wakastajabu,
wakasema, Haijaonekana hivi katika Israeli wakati wo wote. 34 Lakini Mafarisayo
wakasema, Kwa nguvu za mkuu wa pepo atoa pepo.]… Hapa Yesu anamsaidia mtu bubu
ambaye madaktari na familia yake walikuwa na taarifa tofauti ambayo Yesu
aliibadilisha historia na taarifa hizo kuwa uponyaji wa kudumu. Yamkini hata wewe
kwenye ukoo wako yapo mambo ambayo mnayazoea kama yahusuyo ukoo wenu.
Ukimwamini Yesu atabadili historia yako. Mfano 2: MARKO 9:14-18…[Hata
walipowafikia wanafunzi, waliona mkutano mkuu wakiwazunguka, na waandishi
wakijadiliana nao; 15 mara mkutano wote walipomwona walishangaa, wakamwendea
mbio, wakamsalimu. 16 Akawauliza, Mnajadiliana nini nao? 17 Mtu mmoja katika
mkutano akamjibu, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo bubu; 18 na kila
ampagaapo, humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda; nikasema
na wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze.]… Mzazi wa huyu kijana alipogundua
matatizo ya mwanae, alijua kuwa ni pepo na kwamba matukio haya ni ya
kutengenenezwa. Kitendo chake cha kumwaamini Yesu kilimfanya amlete huyu mwanae
kwa Yesu. Matukio ya huyu kijana (mfano wa 2) ni ya kubwagwa chini‼: Kwamba
akiwa kitandani, mapepo yakimpanda yanambwaga chini. Kwamba angekuwa yupo
kwenye ndoa baadae anabwagwa chini (kuachika). Tukio lingine ni kukonda.
Unaweza kutumia virutubisho vyote kwa mwanao lakini bado anaendelea kukonda tu.
Imeandikwa MARKO 9:19-21…[Akawajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nikae
nanyi hata lini? Nichukuliane nanyi hata lini? Mleteni kwangu. 20 Wakamleta
kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaanguka chini,
akagaagaa, akitokwa na povu. 21 Akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini?
Akasema, Tangu utoto.]…Unaweza kuwa na matukio maishani unayoyaona kama ya
kuzaliwa nayo. Ukimwamini Yesu matukio kama haya yanango’oka kwa Jina la Yesu.
Hata kama taabu uliyo nayo ni ya miaka mingi, itaondoka tu. Imeandikwa MARKO
9:22-27…[Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize;
lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia. 23 Yesu akamwambia,
Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. 24 Mara babaye yule kijana akapaza
sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu. 25 Naye Yesu akiona ya
kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe
pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena. 26
Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi
wakasema, Amekufa. 27 Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua naye
akasimama.]…Matukio yaliyofuatia maombi ya Bwana Yesu ni: Kijana kutiwa kifafa
sana, pepo akamtoka, akawa kama amekufa. Jamii yako yaweza kuleta visa
wanapokuona umeletwa kanisanai kuombewa. Wengine watasema unaonekana kama
umekufa. Hata biashara yako yaweza kuonekana kama imekufa baada ya kuombewa.
Wachawi wakitengeneza tukio baya la ubaya au mauti, Mungu hulibadilisha na kuwa
tukio jema la wokovu kwa Jina la Yesu. Bwana ametutuma kutabiri uzima mahali
pasipo na uzima kwa Jina la Yesu. Ezekieli alioneshwa bonde lenye mifupa
mikavu, na Bwana akamwambia aitabirie ile mifupa ili iwe na uzima tena. Baada
ya pale ulitokea upepo ambao uliifanya ile mifupa kuingiwa na nyama na uzima
tena kwa ile mifupa. HASARA ZA MATUKIO YA KICHAWI KUWEPO: 1. Matukio haya
juweza kuzuia kutajwa kwa habaari ya mtu fulani:- Kivipi? Endapo ni ofisini,
habari za mtu zinaweza kuzuiwa zisitajwe. Ni kama mchujo vile unafanyika.
HESABU 23:23….[Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya
Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda
Mungu!]…Matukio ya kichawi yakiondolewa, habari zako zitasemwa. Sasa, habari
zangu zitasemwa. Endapo uchawi na uganga vitaondolewa, habari zako zitaanza
kutangazwa na kusemwa. 2. Matukio ya kichawi huweza kumfanya mtu aache imani:-
MATENDO 13:6-12.. [Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo,
wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake BarYesu; 7 mtu
huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali
akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. 8 Lakini
Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka
kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. 9 Lakini Sauli, ambaye ndiye
Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, 10 akasema, Ewe mwenye kujaa
hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia
za Bwana zilizonyoka? 11 Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa
kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza,
akazungukazunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza. 12 Ndipo
yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya
Bwana.]… Tukio la kichawi hushindana na hatimanzuri ya mtu. Wapo watu wameacha
waume au wake zao ichwai. UKIRI Achia habari zangu kwa Jina la Yesu. Ewe silaha
ya kuacha imani kwa nguvu za kichawi, leo achia kwa Jina la Yesu.
Aliyetengenezea tukio kwa ajili ya misha yangu, nakataa kwa Jina la Yesu. 3.
Matukio ya kichawihuweza kusbabisha magonjwa, hasasra na matatizo: Utagundua
kuwa matukio kama haya yakiwemokatikafamili,matatizo nayo huwa hayakosekani. NJIA
IPI YA KUZISHINDA MATUKIO YA KICHAWI? 1. Ili uweze kushinda, njia nzuri ni
kumpokea Yesu Kristo maishani mwako. Imeandikwa katika YOHANA 1:12..[ Bali wote
waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio
jina lake;]… kwa hiyo,unapokuwa mwana wa Mungu, siyo rahisi kwa wachawi na
mawakala wao kukuletea matukio ya magonjwa, au misiba au mikosi. 2. Njia
nyingine ni kuomba mwenyewe. Ni vizuri uweze kuomba ukiwa mwenyewe, kwa sababu
siyo mara zzote unaweza kuwa na wachungaji karibu na wewe kwa ajiliya kukuombea
unapopatwa na matukio ya kichawi.
No comments:
Post a Comment