BWANA YESU asifiwe. Karibu nikujize jambo
hili. Wanefili maana yake majitu au walioanguka. Hawa walikuwa ni wanadamu
walizaliwa kutokana na mahusiano ya kimapenzi kati ya wana wa MUNGU na binti wa
binadamu. Mwanzo 6:1-5 ''Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana
wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa
ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.BWANA akasema, ROHO yangu haitashindana
na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka
mia na ishirini.Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo
,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo
waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa. BWANA akaona ya kuwa maovu ya
mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni
baya tu sikuzote.''. -wana wa Mungu hawa walikuwa ni malaika walioanguka
(mapepo) ambao walioa wanawake binadamu waliopagagwa kwa nguvu za giza za
mapepo hayo . Uhusiano huu ulisababisha watoto Wanefili. Mwanzo 6:4 '' Nao
Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu
walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu
hodari zamani ,watu wenye sifa.'' shetani kupita mapepo alikuwa anajaribu
kuchafua damu ya binadamu ili kuzuia ujio wa MWOKOZI YESU KRISTO. MUNGU
aliahidi kwamba Masihi atakuja kutoka uzao wa Hawa ambaye ataponda kichwa cha
joka hilo yaani Shetani. Mwanzo 3:15 '' nami nitaweka uadui kati yako na huyo
mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe
utamponda kisigino.'' Hivyo, mapepo au malaika walioasi walitumika ili kujaribu
kuzuia hili na kuchafua ukoo wa binadamu, na kufanya ugumu kwa ajili ya Masihi
asiye na dhambi kuingia duniani kupitia mwanamke. Wanefili walikuwa walikuwa
kizazi kikubwa cha mashujaa maarufu ambao walifanya vitendo vya uovu mkubwa.
ukubwa na nguvu zao zilitokana na mchanganyiko wa “chembe cha za damu” ya
mapepo na zile za binadamu. Biblia inasema kuhusu wao ni kwamba walikuwa
"mashujaa wa zamani, watu wenye sifa" (Mwanzo 6:4). Wanefili walikuwa
si wageni, walikuwa halisi, viumbe wa kimwili zinazozalishwa kutoka muungano wa
malaika waasi na binti wa watu mapepo walirudia tendo la dhambi wakati mwingine
baada ya mafuriko. Hata hivyo, ilifanyika kwa kiasi kidogo kuliko ilivyokuwa
kabla ya mafuriko. Wakati wana wa Israeli walipeleleza nchi ya Kanaani wao
walimpasa Musa taarifa: Hesabu 13:33 "Kisha huko tuliwaona Wanefili, wana
wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi;
nao ndivyo walivyotuona''. Na hata sasa ndio maana ni lazima sana kila mwanadmu
kuokoka kwa kumpokea YESU KRISTO na kuomba maombi au kuombewa maombi ya kujitenga
na kila nguvu za Giza. Mchakato wa BWANA YESU kutuokoa una maana kubwa sana.
Maana mojawapo ya BWANA YESU kutuokoa, Biblia inasema kwamba MUNGU alituhamisha
kutoka nguzu za giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake wa pekee YESU
KRISTO. Wakolosai 1:13 ''Naye(MUNGU) alituokoa katika nguvu za giza,
akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake(YESU ); ambaye
katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;'' Kizazi cha manefili
kilikuja baada ya adamu, kilikuja wakati Wa kabla ya gharika ya Nuhu . ni baada
ya baadhi malaika kuacha enzi yao na kuja kufanya dhambi na wanadamu hivyo
vilivyozaliwa hakikuwa wanadamu Wa kawaida bali ni wanadamu Wa ajabu wakiwemo
wanefili. Ufunuo 12:17 ''Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye
vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za MUNGU, na kuwa na
ushuhuda wa YESU; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.'' -Tangu zamani
shetani amekasirika dhidi ya mwanamke na amedhamiria kufanya vita juu ya uzao
wa mwanamke, vita hiyo ni kuhakikisha uzao wa mwanamke haumpendezi MUNGU.
Wanefili ni zao la hasira ya shetani kwa uzao wa mwanamke. Lakini ashukuriwe
MUNGU kwa BWANA wetu YESU KRISTO kuja kutuokoa. Kitendo cha Malaika kuasi
mbinguni na kuja kufanya uasherati na wanadamu ili kupelekea kuzaliwa kwa watu
walio na ushetani ndani yao Lilikuwa ni kosa kubwa kwa MUNGU. malaika kuacha
enzi yao na kuja kufanya dhambi, malaika hao waliadhibiwa na wako kifungoni
wakisubiri jehanamu. Yuda 1:6 " Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe,
lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele
chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu. " Unefili ulikuwa ni mkakati wa
kuhakikisha wanadamu hawaendi kuishi katika uzima wa milele lakini ashukuriwe
BWANA YESU kwa kuja kutukomboa na kututoa katika kila nguvu za giza na
tunawekwa huru kwa damu ya YESU KRISTO. Warumi 6:22-13 ''Lakini sasa mkiisha
kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa MUNGU, mnayo
faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele. Kwa maana
mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika
KRISTO YESU BWANA wetu.'' Damu ya YESU KRISTO ina uwezo wa kututenga na kila
nguvu za giza. BWANA YESU akikuweka huru hakika utakuwa huru. Yohana 8:36 ''
Basi Mwana(YESU) akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.'' Mapepo ni wanefili
ambao hawatakiwi kuishi ndani ya mtu. mapepo yako kifungoni sasa maana yake
kuna vitu MUNGU ameyazuilia kufanya kwa wanadamu lakini mwanadamu akiwa mbali
na KRISTO anaweza kuvamiwa na mapepo na mapepo hayo yatamfanya mwanadamu huyo
kuwa shujaa katika kutenda dhambi. Kuna watu leo ni mashujaa wa
kipepo(kinefili) wa kunywa pombe nyingi. Kuna watu leo ni mashujaa wa kipepo wa
kubadili wanawake/wanaume kama nguo. huo ni unefili unaotakiwa kuondolewa kwa
jina la YESU KRISTO ndipo mtu atakuwa huru tena bila kuongozwa na nguvu za
giza. 2 Kor 5:17 '' Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe
kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.'' Naamini kabisa kuna kitu
umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha
ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka. Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee
leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu. Kama wewe ni mtu
wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua
kumpendeza MUNGU kuanzia leo. Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha
kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa
waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako. ubarikiwe sana pia kwa kujifunza
masomo yangu. Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula. 0714252292.
mabula1986@gmail.com Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.
WANEFILI NA JINSI
WALIVYOTOKEA DUNIANI.
Na Mtumishi Peter Mabula.
BWANA YESU asifiwe.
Karibu nikujize jambo hili.
Wanefili maana yake majitu au walioanguka.
Hawa walikuwa ni wanadamu walizaliwa kutokana na mahusiano ya
kimapenzi kati ya wana wa MUNGU na binti wa binadamu.
Mwanzo 6:1-5 ''Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana
wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu
ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.BWANA
akasema, ROHO yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye
naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.Nao
Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu
walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa
watu hodari zamani ,watu wenye sifa. BWANA akaona ya kuwa maovu ya
mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni
mwake ni baya tu sikuzote.''.
-wana wa Mungu hawa walikuwa ni malaika walioanguka (mapepo) ambao
walioa wanawake binadamu waliopagagwa kwa nguvu za giza za mapepo hayo .
Uhusiano huu ulisababisha watoto Wanefili.
Mwanzo 6:4 '' Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya
hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao
wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa.''
shetani kupita mapepo alikuwa anajaribu kuchafua damu ya binadamu ili
kuzuia ujio wa MWOKOZI YESU KRISTO.
MUNGU aliahidi kwamba Masihi atakuja kutoka uzao wa Hawa ambaye
ataponda kichwa cha joka hilo yaani Shetani.
Mwanzo 3:15 '' nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati
ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda
kisigino.''
Hivyo, mapepo au malaika walioasi walitumika ili kujaribu kuzuia hili
na kuchafua ukoo wa binadamu, na kufanya ugumu kwa ajili ya Masihi asiye
na dhambi kuingia duniani kupitia mwanamke.
Wanefili walikuwa walikuwa kizazi kikubwa cha mashujaa maarufu ambao
walifanya vitendo vya uovu mkubwa.
ukubwa na nguvu zao zilitokana na mchanganyiko wa “chembe cha za damu”
ya mapepo na zile za binadamu. Biblia inasema kuhusu wao ni kwamba
walikuwa "mashujaa wa zamani, watu wenye sifa" (Mwanzo 6:4).
Wanefili walikuwa si wageni, walikuwa halisi, viumbe wa kimwili
zinazozalishwa kutoka muungano wa malaika waasi na binti wa watu
mapepo walirudia tendo la dhambi wakati mwingine baada ya mafuriko.
Hata hivyo, ilifanyika kwa kiasi kidogo kuliko ilivyokuwa kabla ya
mafuriko. Wakati wana wa Israeli walipeleleza nchi ya Kanaani wao
walimpasa Musa taarifa:
Hesabu 13:33 "Kisha huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka
kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo
walivyotuona''.
Na hata sasa ndio maana ni lazima sana kila mwanadmu kuokoka kwa
kumpokea YESU KRISTO na kuomba maombi au kuombewa maombi ya kujitenga na
kila nguvu za Giza.
Mchakato wa BWANA YESU kutuokoa una maana kubwa sana.
Maana mojawapo ya BWANA YESU kutuokoa, Biblia inasema kwamba MUNGU
alituhamisha kutoka nguzu za giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana
wake wa pekee YESU KRISTO.
Wakolosai 1:13 ''Naye(MUNGU) alituokoa katika nguvu za giza,
akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake(YESU );
ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;''
Kizazi cha manefili kilikuja baada ya adamu, kilikuja wakati Wa kabla
ya gharika ya Nuhu . ni baada ya baadhi malaika kuacha enzi yao na kuja
kufanya dhambi na wanadamu hivyo vilivyozaliwa hakikuwa wanadamu Wa
kawaida bali ni wanadamu Wa ajabu wakiwemo wanefili.
Ufunuo 12:17 ''Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye
vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za MUNGU, na kuwa na
ushuhuda wa YESU; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.''
-Tangu zamani shetani amekasirika dhidi ya mwanamke na amedhamiria
kufanya vita juu ya uzao wa mwanamke, vita hiyo ni kuhakikisha uzao wa
mwanamke haumpendezi MUNGU.
Wanefili ni zao la hasira ya shetani kwa uzao wa mwanamke.
Lakini ashukuriwe MUNGU kwa BWANA wetu YESU KRISTO kuja kutuokoa.
Kitendo cha Malaika kuasi mbinguni na kuja kufanya uasherati na wanadamu
ili kupelekea kuzaliwa kwa watu walio na ushetani ndani yao Lilikuwa ni
kosa kubwa kwa MUNGU.
malaika kuacha enzi yao na kuja kufanya dhambi, malaika hao
waliadhibiwa na wako kifungoni wakisubiri jehanamu.
Yuda 1:6 " Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha
makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya
giza kwa hukumu ya siku ile kuu. "
Unefili ulikuwa ni mkakati wa kuhakikisha wanadamu hawaendi kuishi
katika uzima wa milele lakini ashukuriwe BWANA YESU kwa kuja kutukomboa
na kututoa katika kila nguvu za giza na tunawekwa huru kwa damu ya YESU
KRISTO.
Warumi 6:22-13 ''Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na
dhambi, na kufanywa watumwa wa MUNGU, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa,
na mwisho wake ni uzima wa milele. Kwa maana mshahara wa dhambi ni
mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU BWANA
wetu.''
Damu ya YESU KRISTO ina uwezo wa kututenga na kila nguvu za giza.
BWANA YESU akikuweka huru hakika utakuwa huru.
Yohana 8:36 '' Basi Mwana(YESU) akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli
kweli.''
Mapepo ni wanefili ambao hawatakiwi kuishi ndani ya mtu.
mapepo yako kifungoni sasa maana yake kuna vitu MUNGU ameyazuilia
kufanya kwa wanadamu lakini mwanadamu akiwa mbali na KRISTO anaweza
kuvamiwa na mapepo na mapepo hayo yatamfanya mwanadamu huyo kuwa shujaa
katika kutenda dhambi.
Kuna watu leo ni mashujaa wa kipepo(kinefili) wa kunywa pombe nyingi.
Kuna watu leo ni mashujaa wa kipepo wa kubadili wanawake/wanaume kama
nguo. huo ni unefili unaotakiwa kuondolewa kwa jina la YESU KRISTO ndipo
mtu atakuwa huru tena bila kuongozwa na nguvu za giza.
2 Kor 5:17 '' Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe
kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.''
Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni
wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi
maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba
okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako ,
nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia
kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
No comments:
Post a Comment