Hesabu 22: 1-6 “Kisha wana wa Israeli wakasafiri na kupanga
katika nchi tambarare za Moabu ng'ambo ya pili ya Yordani karibu ya Yeriko. Na
Balaki mwana wa Sipori akaona mambo yote ambayo Israeli wamewatendea Waamori.
Moabu akawaogopa hao watu sana, kwa kuwa walikuwa wengi; Moabu akafadhaika kwa
sababu ya wana wa Israeli. Moabu akawaambia wazee wa Midiani, Sasa jeshi hili
la watu litaramba vitu vyote vinavyotuzunguka, kama vile ng'ombe arambavyo
majani ya mashamba. Na Balaki, mwana wa Sipori, alikuwa mfalme wa Moabu zamani
zile. Basi akatuma wajumbe kwa Balaamu mwana wa Beori, hata Pethori, ulio kando
ya Mto, mpaka nchi ya wana wa watu wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna
watu waliotoka Misri; tazama, wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili
mimi. Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu
kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika
nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye
umlaaniye hulaaniwa.” Baalam alikuwa mchawi aliyetaka kuwalaani wana wa Israei.
Wana wa Israeli walikuwa wameshinda kila walipokuwa wakafika mahali. Wakakutana
na mfalme wa moabu ambaye alimkodisha baalam ili awalaani wasije wakamshinda.
“Ukilaaniwa hata kama ulikuwa unaelekea kushinda unashindwa.” Baalam alijaribu
kuwalaani watu wa Bwana lakini hawakulaanika. Yoshua 13:22 “ufalme wote wa Ogu
uliokuwa katika Bashani, huyo aliyekuwa akitawala katika Ashtarothi na katika
Edrei (huyo alisalia katika mabaki ya wale Warefai); kwa kuwa Musa aliwapiga
hao na kuwafukuza. Pamoja na hayo wana wa Israeli hawakuwafukuza Wageshuri,
wala Wamaaka; lakini Wageshuri na Wamaaka wamekaa kati ya Israeli, hata siku
hii ya leo.” Hesabu 22:7 “Wazee wa Moabu, na wazee wa Midiani, wakaenda,
wakichukua ujira wa uganga mikononi mwao; wakamfikilia Balaamu, wakamwambia
maneno ya Balaki.” Kuna ujira wa uganga ambao ni mahitaji ya mchawi anayoyataka
ili atimize mambo yake. Huyu baaalam mchawi alichukua ujira ili awalaani wana
wa Israeli. Kwenye maisha yetu ya kila siku inawezekana kuna mtu anakuona
umefanikiwa sana kwenye ndoa, kazi, biashara akakuonea wivu na kuamua kwenda
kwa mganga wa kienyeji na kutoa ujira ili ulaaniwe ushuke chini na kushindwa
kuendelea kufanikiwa. Hesabu 23:1 “Balaamu akamwambia Balaki, Nijengee hapa
madhabahu saba, ukaniandalie hapa ng'ombe waume saba, na kondoo waume saba.
Balaki akafanya kama Balaamu alivyonena. Balaki na Balaamu wakatoa sadaka,
ng'ombe mume mmoja na kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu. Balaamu
akamwambia Balaki, Simama karibu na sadaka yako, nami nitakwenda, labda Bwana
atakuja kuonana nami; na lo lote atakalonionyesha nitakuambia. Akaenda hata
mahali peupe juu ya kilima. Mungu akakutana na Balaamu; naye Balaamu
akamwambia, Nimetengeneza madhabahu saba, nami nimetoa sadaka ng'ombe mume
mmoja na kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu. Bwana akatia neno katika
kinywa chake Balaamu, akasema, Umrudie Balaki; ukaseme maneno haya.” Kwenye
maisha ya kawaida wachawi nao wana wana madhabahu za kutoa laana ili ziwapate
watu waliokusudiwa. Laana ya kichawi hutokea kwenye madhabahu ya kichawi.
Baalam alianza kuangalia kwenye ulimwengu wa rohoni ili shetani aje na kuitamka
ile laana kwa wana wa Israeli lakini Yehova aliingilia kati na kuizuia laana
ile isifanikiwe kutoka kwenye madhabahu ya kishetani ya baali. Baalam
alijitahidi ili awalaani wana wa Israeli lakini mdomoni mwake ilitoka Baraka
kwasababu Mungu aliingilia madhabahu yake na kumfanya atamke baraka. Hii
inamaanisha hata kwenye maisha ya kila siku yeyote anayetaka kukulaani wewe au
biashara yako au ndoa yako au kazi yako laana isiyo na sababu haiwezi kukupata
kwa jina la Yesu, baalam ahamisha madhabahu ili aweze kuwalaani wana wa Israeli
vizuri lakini kila alipokwenda aliishia kuwabariki. Kila madhabahu iliyo jengwa
ina jina lake, jina la madhabahu ndilo linalofanya madhabahu iwe na matokeo
Fulani yanayoendana na jina lake. Wana wa Israeli walisafiri kwa miaka 40
kufika kwenye nchi ya ahadi. Ukiangalia kwenye maisha ya kila siku mtu anaweza
kuchelewa kuolewa au kufanikiwa kwasababu ya kudharau mambo madogo madogo
ambayo ni ya Mungu lakini yanaonekana kama mambo ya kitoto kwenye macho ya
wanadamu, jambo lingine mtu anaweza kuchelewa ni kujifanya anajua kila kitu.
Mambo ya Mungu ni kama mambo ya kitoto na ukijfanya unayajua sana unaweza
ukajikuta unaharibikiwa kabisa. Kwenye maisha ya kila siku Mungu hujidhihirisha
kwenye mambo madogo na manyonge ambayo kibinadamu yanadharaulika. Wana wa
Israeli walichelewa kufika kwenye nchi ya ahadi sababu walijifanya wanamjua
sana na Mungu ndipo akaamua kuwachelewesha kwa miaka 40 mpaka ule ujuaji wao
uishe. Mungu alitaka Misri iwatoke ndani yao kwamaana kama walikuwa wakifanya
hivi na hivi waache wafanye hivi. Sababu nyingine Mungu alitaka kuwafundisha
vita ndiomaana aliwachelewesha kufika kwenye nchi ya ahadi. Aina za wokovu Kuna
aina ya wokovu ambao mtu anajisimamia mwenyewe mpaka anasimama imara. Wokovu
mwingine ni ule mtu anafuatiliwa mpaka anasimama na kujisimamia mwenyewe,
wokovu mwingine ni ule ambao mtu anafuatilia mambo fulani fulani ili ayapate na
akishayapata anaondoka na kuendelea na mambo yake. Kuna baadhi ya watu
wanawafuatilia watu wa kuwaoa/olewa nao sababu wanajua wakitaka kupata watu
wazuri wa kuoana nao wanapatikana kanisani hivyo wanajifanya nao wameokoka wako
ndani ya wokovu ili wapate mambo yanayofanana na hayo. Kuna ule wokovu wa asili
ambao Mungu anakupa na anakupa ili kukutengeneza uwe mtu wa vita na anakuwa
anakucheleweshea baadhi ya vitu usivipate ili akufundishe uwe mtu wa vita na
ukija kuvipata unakuwa una uwezo wa kuviongoza na kuvimiliki. Mungu ni Mungu wa
vita sisi pia tunatakiwa tuwe watu wa vita Waefeso 6: 12 “Kwa maana kushindana
kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya
wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”
Maana yake tunapopita kuna viumbe wa giza kwenye ulimwengu wa rohoni kwa maana
mashetani na mapepo ambayo yanatuzuia tusiende kule tunapotaka kwenda hivyo hiyo
ndiyo vita yetu tuliyo nayo. Ule uwezo wako wa kuwaendea na kuwapiga kwenye
ulimwengu wa rohoni ndivyo uwezekano wako wa kumili vilevile kama ulivyo shinda
baadaye. Sisi ni vinywa vya Bwana na mabalozi wa Mungu hapa duniani. Ukiri
“Katika jina la Yesu laana ya wachawi inayotokea kwenye madhabahu haitanipata
mimi kwa jina la yesu.” Kuna baadhi ya koo zimejengewa madhabahu za kumilikiwa
ambapo familia zinakuwa zinamilikiwa na balaa, ajali, magonjwa, zingine
zinakuwa za kuzuia mafanikio na vitu mbalimbali na unapofanikiwa kuzibomoa
madhabahu hizo ndipo unapenya kwenye maisha yako. Kuna madhabahu ambazo
zimeshikilia roho za watu ambapo unaweza kumwona mtu mjanja kweli lakini
ukimwangalia kwenye mambo ya kufanikiwa hana kitu. Kuna baadhi ya mambo huwezi
kuyachangamkia sababu umelazwa kwenye madhabahu. Matendo 17:23 “Kwa sababu
nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada yenu, naliona
madhabahu iliyoandikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi mimi
nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua.” Kwenye
madhabahu hii inategemea kuhani anasema nini sababu Mungu wake hajulikani.
Maombi “Katika jina la Yesu ninaamuru kila madhabahu iliyonilaza na aliyenilaza
ninaivunja kwa jina la Yesu, ninawaponda na kuwaangamiza makuhani wa madhabahu
kwa jina la Yesu, ninazinyamazisha kafara za madhabahu kwa damu ya mwanakondoo
katika jina la Yesu. Amen” Mwanzo 33:20 “Akajenga huko madhabahu, akaiita,
El-elohe-Israeli (El-elohe-Israeli maana yake ni Mungu, Mungu wa Israeli).”
Neno Israeli maana yake ni “aliyeshindana akashinda”, Unaweza kuona shetani
alipotaka kuiteka nchi alibomoa madhabahu kwanza. Duniani wachawi wanajua kuna
watu ukiwasonga’songa uhusihano wa watu wengi na Mungu utaharibika Warumi11:3
“Bwana, wamewaua manabii wako, wamezibomoa madhabahu zako, nami nimesalia peke
yangu, nao wananitafuta roho yangu. Lakini ile jawabu ya Mungu yamwambiaje?
Nimejisazia watu elfu saba wasiopiga goti mbele ya Baali. Basi ni vivi hivi
wakati huu wa sasa, yako mabaki waliochaguliwa kwa neema.” Kuna madhabahu ya
usalama ambayo mtu anaitengeneza ili awe salama, biashara yake iwe salama,
familia yake iwe salama na unaweza kuona kuna baadhi ya familia ambazo watu
wanaishi ndani yake na wamejiwekea ulinzi kutoka kwenye madhabahu hizi ili
kujilinda. Ufalme wa shetani unafanya kazi na baadaye unakuumbua, shetani
haukuachi hivihivi unakuwa unatoa kafara kwenye madhabahu hizo mpaka unaishiwa
unafariki wewe mwenyewe. Kutoka 17:15 “Musa akajenga madhabahu, akaiita jina
lake Yehova-nisi (Yehova-nisi maana yake ni Bwana ni bendera yangu); akasema,
Bwana ameapa; Bwana atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi.” Amaleki
ni kabila ambalo kipindi wana wa Israeli wakiongozwa na Musa walipita kwenye
nchi yao ambapo wana wa Israeli waliwaomba wapiti kwa Amani bila kushika
chochote chao wala maji yao wala udongo wao ni kupita tu lakini amaleki
walikataa na kujaribu kuwazuia wasipite na ikumbukw Bwana aliwalaani amaleki
kizazi hadi kizazi na leo hii Mungu anafanya vita na amaleki wa Tanzania
anayewatesa watu na ndoa zao, anayewatesa watu na ajira zao, anayewatesa watu
na uchumi wao, Mungu ameapa kufanya nao vita na wameshapigwa kwa jina la Yesu.
Musa alipeleka barua ya kuwaomba kupita katika njia kuu kwenda kwenye nchi ya
ahadi hivyo watulie bila kuogopa jinsi walivyokuwa wanaonekana lakini
walipokataa Mungu aliwatia wana waIsraeli nguvu wakawashinda amaleki na kusonga
mbele kwenye nchi ya ahadi. “Biblia imetufundisha mambo matatu la kwanza
tunatakiwa tutambue yale tunayotakiwa kuyafanya “iweni watakatifu kama mimi nilivyo
mtakatifu”, “hamkosi kuzitambua hila zake adui”, pili Biblia imetufundisha
kutoka kwa wenzetu ambao walifanya makosa walipokuwa ndani ya wokovu ili
kupitia yale makosa yao sisi tujifunze na Tatu Biblia imetufundisha yale ambayo
hayakutimia kwa mikono ya akina Petro, Yohana na manabii wengine sisi tuyatende
kama Askari wa Mbinguni, Mabalozi wa mbinguni hapa duniani”
MADHABAHU YA LAANA
Na Askofu mkuu Josephat Gwajima.
Hesabu 22: 1-6
“Kisha wana wa Israeli wakasafiri na kupanga katika nchi tambarare za
Moabu ng'ambo ya pili ya Yordani karibu ya Yeriko. Na Balaki mwana wa
Sipori akaona mambo yote ambayo Israeli wamewatendea Waamori. Moabu
akawaogopa hao watu sana, kwa kuwa walikuwa wengi; Moabu akafadhaika kwa
sababu ya wana wa Israeli. Moabu akawaambia wazee wa Midiani, Sasa
jeshi hili la watu litaramba vitu vyote vinavyotuzunguka, kama vile
ng'ombe arambavyo majani ya mashamba. Na Balaki, mwana wa Sipori,
alikuwa mfalme wa Moabu zamani zile. Basi akatuma wajumbe kwa Balaamu
mwana wa Beori, hata Pethori, ulio kando ya Mto, mpaka nchi ya wana wa
watu wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna watu waliotoka Misri;
tazama, wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili mimi. Basi,
njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda
mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi
yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye
umlaaniye hulaaniwa.”
Baalam alikuwa mchawi aliyetaka kuwalaani wana wa Israei. Wana wa
Israeli walikuwa wameshinda kila walipokuwa wakafika mahali. Wakakutana
na mfalme wa moabu ambaye alimkodisha baalam ili awalaani wasije
wakamshinda. “Ukilaaniwa hata kama ulikuwa unaelekea kushinda
unashindwa.” Baalam alijaribu kuwalaani watu wa Bwana lakini
hawakulaanika.
Yoshua 13:22
“ufalme wote wa Ogu uliokuwa katika Bashani, huyo aliyekuwa akitawala
katika Ashtarothi na katika Edrei (huyo alisalia katika mabaki ya wale
Warefai); kwa kuwa Musa aliwapiga hao na kuwafukuza. Pamoja na hayo wana
wa Israeli hawakuwafukuza Wageshuri, wala Wamaaka; lakini Wageshuri na
Wamaaka wamekaa kati ya Israeli, hata siku hii ya leo.”
Hesabu 22:7
“Wazee wa Moabu, na wazee wa Midiani, wakaenda, wakichukua ujira wa
uganga mikononi mwao; wakamfikilia Balaamu, wakamwambia maneno ya
Balaki.”
Kuna ujira wa uganga ambao ni mahitaji ya mchawi anayoyataka ili atimize
mambo yake. Huyu baaalam mchawi alichukua ujira ili awalaani wana wa
Israeli. Kwenye maisha yetu ya kila siku inawezekana kuna mtu anakuona
umefanikiwa sana kwenye ndoa, kazi, biashara akakuonea wivu na kuamua
kwenda kwa mganga wa kienyeji na kutoa ujira ili ulaaniwe ushuke chini
na kushindwa kuendelea kufanikiwa.
Hesabu 23:1
“Balaamu akamwambia Balaki, Nijengee hapa madhabahu saba, ukaniandalie
hapa ng'ombe waume saba, na kondoo waume saba. Balaki akafanya kama
Balaamu alivyonena. Balaki na Balaamu wakatoa sadaka, ng'ombe mume mmoja
na kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu. Balaamu akamwambia Balaki,
Simama karibu na sadaka yako, nami nitakwenda, labda Bwana atakuja
kuonana nami; na lo lote atakalonionyesha nitakuambia. Akaenda hata
mahali peupe juu ya kilima. Mungu akakutana na Balaamu; naye Balaamu
akamwambia, Nimetengeneza madhabahu saba, nami nimetoa sadaka ng'ombe
mume mmoja na kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu. Bwana akatia neno
katika kinywa chake Balaamu, akasema, Umrudie Balaki; ukaseme maneno
haya.”
Kwenye maisha ya kawaida wachawi nao wana wana madhabahu za kutoa laana
ili ziwapate watu waliokusudiwa. Laana ya kichawi hutokea kwenye
madhabahu ya kichawi. Baalam alianza kuangalia kwenye ulimwengu wa
rohoni ili shetani aje na kuitamka ile laana kwa wana wa Israeli lakini
Yehova aliingilia kati na kuizuia laana ile isifanikiwe kutoka kwenye
madhabahu ya kishetani ya baali. Baalam alijitahidi ili awalaani wana wa
Israeli lakini mdomoni mwake ilitoka Baraka kwasababu Mungu aliingilia
madhabahu yake na kumfanya atamke baraka. Hii inamaanisha hata kwenye
maisha ya kila siku yeyote anayetaka kukulaani wewe au biashara yako au
ndoa yako au kazi yako laana isiyo na sababu haiwezi kukupata kwa jina
la Yesu, baalam ahamisha madhabahu ili aweze kuwalaani wana wa Israeli
vizuri lakini kila alipokwenda aliishia kuwabariki.
Kila madhabahu iliyo jengwa ina jina lake, jina la madhabahu ndilo
linalofanya madhabahu iwe na matokeo Fulani yanayoendana na jina lake.
Wana wa Israeli walisafiri kwa miaka 40 kufika kwenye nchi ya ahadi.
Ukiangalia kwenye maisha ya kila siku mtu anaweza kuchelewa kuolewa au
kufanikiwa kwasababu ya kudharau mambo madogo madogo ambayo ni ya Mungu
lakini yanaonekana kama mambo ya kitoto kwenye macho ya wanadamu, jambo
lingine mtu anaweza kuchelewa ni kujifanya anajua kila kitu. Mambo ya
Mungu ni kama mambo ya kitoto na ukijfanya unayajua sana unaweza
ukajikuta unaharibikiwa kabisa. Kwenye maisha ya kila siku Mungu
hujidhihirisha kwenye mambo madogo na manyonge ambayo kibinadamu
yanadharaulika.
Wana wa Israeli walichelewa kufika kwenye nchi ya ahadi sababu
walijifanya wanamjua sana na Mungu ndipo akaamua kuwachelewesha kwa
miaka 40 mpaka ule ujuaji wao uishe. Mungu alitaka Misri iwatoke ndani
yao kwamaana kama walikuwa wakifanya hivi na hivi waache wafanye hivi.
Sababu nyingine Mungu alitaka kuwafundisha vita ndiomaana
aliwachelewesha kufika kwenye nchi ya ahadi.
Aina za wokovu
Kuna aina ya wokovu ambao mtu anajisimamia mwenyewe mpaka anasimama
imara. Wokovu mwingine ni ule mtu anafuatiliwa mpaka anasimama na
kujisimamia mwenyewe, wokovu mwingine ni ule ambao mtu anafuatilia mambo
fulani fulani ili ayapate na akishayapata anaondoka na kuendelea na
mambo yake. Kuna baadhi ya watu wanawafuatilia watu wa kuwaoa/olewa nao
sababu wanajua wakitaka kupata watu wazuri wa kuoana nao wanapatikana
kanisani hivyo wanajifanya nao wameokoka wako ndani ya wokovu ili wapate
mambo yanayofanana na hayo. Kuna ule wokovu wa asili ambao Mungu
anakupa na anakupa ili kukutengeneza uwe mtu wa vita na anakuwa
anakucheleweshea baadhi ya vitu usivipate ili akufundishe uwe mtu wa
vita na ukija kuvipata unakuwa una uwezo wa kuviongoza na kuvimiliki.
Mungu ni Mungu wa vita sisi pia tunatakiwa tuwe watu wa vita
Waefeso 6: 12
“Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya
falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo
wabaya katika ulimwengu wa roho.”
Maana yake tunapopita kuna viumbe wa giza kwenye ulimwengu wa rohoni kwa
maana mashetani na mapepo ambayo yanatuzuia tusiende kule tunapotaka
kwenda hivyo hiyo ndiyo vita yetu tuliyo nayo. Ule uwezo wako wa
kuwaendea na kuwapiga kwenye ulimwengu wa rohoni ndivyo uwezekano wako
wa kumili vilevile kama ulivyo shinda baadaye.
Sisi ni vinywa vya Bwana na mabalozi wa Mungu hapa duniani.
Ukiri
“Katika jina la Yesu laana ya wachawi inayotokea kwenye madhabahu
haitanipata mimi kwa jina la yesu.”
Kuna baadhi ya koo zimejengewa madhabahu za kumilikiwa ambapo familia
zinakuwa zinamilikiwa na balaa, ajali, magonjwa, zingine zinakuwa za
kuzuia mafanikio na vitu mbalimbali na unapofanikiwa kuzibomoa madhabahu
hizo ndipo unapenya kwenye maisha yako. Kuna madhabahu ambazo
zimeshikilia roho za watu ambapo unaweza kumwona mtu mjanja kweli lakini
ukimwangalia kwenye mambo ya kufanikiwa hana kitu. Kuna baadhi ya mambo
huwezi kuyachangamkia sababu umelazwa kwenye madhabahu.
Matendo 17:23
“Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada
yenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, KWA MUNGU
ASIYEJULIKANA. Basi mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi
mnamwabudu bila kumjua.”
Kwenye madhabahu hii inategemea kuhani anasema nini sababu Mungu wake
hajulikani.
Maombi
“Katika jina la Yesu ninaamuru kila madhabahu iliyonilaza na aliyenilaza
ninaivunja kwa jina la Yesu, ninawaponda na kuwaangamiza makuhani wa
madhabahu kwa jina la Yesu, ninazinyamazisha kafara za madhabahu kwa
damu ya mwanakondoo katika jina la Yesu. Amen”
Mwanzo 33:20
“Akajenga huko madhabahu, akaiita, El-elohe-Israeli (El-elohe-Israeli
maana yake ni Mungu, Mungu wa Israeli).”
Neno Israeli maana yake ni “aliyeshindana akashinda”, Unaweza kuona
shetani alipotaka kuiteka nchi alibomoa madhabahu kwanza. Duniani
wachawi wanajua kuna watu ukiwasonga’songa uhusihano wa watu wengi na
Mungu utaharibika
Warumi11:3 “Bwana, wamewaua manabii wako, wamezibomoa madhabahu zako,
nami nimesalia peke yangu, nao wananitafuta roho yangu. Lakini ile
jawabu ya Mungu yamwambiaje? Nimejisazia watu elfu saba wasiopiga goti
mbele ya Baali. Basi ni vivi hivi wakati huu wa sasa, yako mabaki
waliochaguliwa kwa neema.”
Kuna madhabahu ya usalama ambayo mtu anaitengeneza ili awe salama,
biashara yake iwe salama, familia yake iwe salama na unaweza kuona kuna
baadhi ya familia ambazo watu wanaishi ndani yake na wamejiwekea ulinzi
kutoka kwenye madhabahu hizi ili kujilinda. Ufalme wa shetani unafanya
kazi na baadaye unakuumbua, shetani haukuachi hivihivi unakuwa unatoa
kafara kwenye madhabahu hizo mpaka unaishiwa unafariki wewe mwenyewe.
Kutoka 17:15 “Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi
(Yehova-nisi maana yake ni Bwana ni bendera yangu); akasema, Bwana
ameapa; Bwana atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi.”
Amaleki ni kabila ambalo kipindi wana wa Israeli wakiongozwa na Musa
walipita kwenye nchi yao ambapo wana wa Israeli waliwaomba wapiti kwa
Amani bila kushika chochote chao wala maji yao wala udongo wao ni kupita
tu lakini amaleki walikataa na kujaribu kuwazuia wasipite na ikumbukw
Bwana aliwalaani amaleki kizazi hadi kizazi na leo hii Mungu anafanya
vita na amaleki wa Tanzania anayewatesa watu na ndoa zao, anayewatesa
watu na ajira zao, anayewatesa watu na uchumi wao, Mungu ameapa kufanya
nao vita na wameshapigwa kwa jina la Yesu. Musa alipeleka barua ya
kuwaomba kupita katika njia kuu kwenda kwenye nchi ya ahadi hivyo
watulie bila kuogopa jinsi walivyokuwa wanaonekana lakini walipokataa
Mungu aliwatia wana waIsraeli nguvu wakawashinda amaleki na kusonga
mbele kwenye nchi ya ahadi.
“Biblia imetufundisha mambo matatu la kwanza tunatakiwa tutambue yale
tunayotakiwa kuyafanya “iweni watakatifu kama mimi nilivyo mtakatifu”,
“hamkosi kuzitambua hila zake adui”, pili Biblia imetufundisha kutoka
kwa wenzetu ambao walifanya makosa walipokuwa ndani ya wokovu ili
kupitia yale makosa yao sisi tujifunze na Tatu Biblia imetufundisha yale
ambayo hayakutimia kwa mikono ya akina Petro, Yohana na manabii wengine
sisi tuyatende kama Askari wa Mbinguni, Mabalozi wa mbinguni hapa
duniani”
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
No comments:
Post a Comment