BWANA YESU asifiwe ndugu yangu.
Nakukaribisha tujifunze jinsi ya kudai haki zetu mbele za MUNGU. Tunajua
tunadai haki kwa nani? Haki zetu tunazidai pale ambapo tunauhitaji wa jambo
Fulani mbele za MUNGU. Ni lazima tumjue vyema tunayemdai. Je tunasifa za kudai
hicho tunachotaka? Isaya 54:17 (Kila silaha itakayofanyika juu yako
haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa
mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu
mimi, asema BWANA. ) Watu wengi hatujui jinsi ya kudai haki zetu mbele za
MUNGU, Watu wengi hatufahamu tudai nini, Watu wengi hua tunajaribu tu kudai
lakini hatuna imani ya kupokea na wengine hatujampokea BWANA YESU ambaye ndio
chanzo cha haki yetu yote hivyo hatuwezi kupokea. Kuna haki zinafahamika
zinafahamika na kuna haki hatuzijui. Muda mwingi unawaza ‘’hivi MUNGU
hanioni?’’ Wakati mwingine unawaza ‘’Mbona Fulani kafanikiwa?’’ Yeremia 1:19 (
Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema
BWANA, ili nikuokoe. ) Tatizo sio kujua ila tatizo ni kutambua haki yako mbele
za MUNGU. Tujikubali kwa maneno na kwa matendo pia. Haki ya MUNGU haionekani
kwa macho hadi pale haki yako itakapofanya kazi ndio utaona matokeo mazuri.
Kutoka 15:1-18(Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia BWANA wimbo huu
wakanena, na kusema, Nitamwimbia BWANA, kwa maana ametukuka sana; Farasi na
mpanda farasi amewatupa baharini. BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye
amekuwa wokovu wangu. Yeye ni MUNGU wangu, nami nitamsifu; Ni MUNGU wa baba
yangu, nami nitamtukuza. BWANA ni mtu wa vita, BWANA ndilo jina lake. Magari ya
Farao na jeshi lake amewatupa baharini, Maakida yake wateule wamezama katika
bahari ya Shamu. Vilindi vimewafunikiza, Walizama vilindini kama jiwe. BWANA,
mkono wako wa kuume umepata fahari ya uwezo, BWANA, mkono wako wa kuume
wawaseta-seta adui. Kwa wingi wa ukuu wako wawaangusha chini wanaokuondokea,
Wapeleka hasira yako, nayo huwateketeza kama mabua makavu. Kwa upepo wa mianzi
ya pua yako maji yalipandishwa, Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa chungu,
Vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari. Adui akasema, Nitafuatia,
nitapata, nitagawanya nyara, Nafsi yangu itashibishwa na wao; Nitaufuta upanga
wangu, mkono wangu utawaangamiza. Ulivuma kwa upepo wako, bahari ikawafunikiza;
Wakazama kama risasi ndani ya maji makuu. Ee BWANA, katika miungu ni nani aliye
kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa
katika sifa zako, mfanya maajabu? Ulinyosha mkono wako wa kuume, Nchi
ikawameza. Wewe kwa rehema zako umewaongoza watu uliowakomboa, Kwa uweza wako
uliwaelekeza hata makao yako matakatifu. Kabila za watu wamesikia,
wanatetemeka, Wakaao Ufilisti utungu umewashika. Ndipo majumbe wa Edomu
wakashangaa, Watu wa Moabu wenye nguvu tetemeko limewapata, Watu wote wakaao
Kanaani wameyeyuka. Hofu na woga umewaangukia; Kwa uweza wa mkono wako wanakaa
kimya kama jiwe; Hata watakapovuka watu wako, Ee BWANA, Hata watakapovuka watu
wako uliowanunua. Utawaingiza, na kuwapanda katika mlima wa urithi wako, Mahali
pale ulipojifanyia, Ee BWANA, ili upakae, Pale patakatifu ulipopaweka imara,
BWANA, kwa mikono yako. BWANA atatawala milele na milele. ). -Maandiko hapo juu
yanaonyesha Musa na wana wa Israeli walitambua haki yako mbele za MUNGU . -Hapo
juu inaonyesha kwamba huwezi kumsifu mtu usiyemuona. -Itambue haki yak oleo kwa
MUNGU. -BWANA amkekupa haki tena, unaweza kuomba lolote kwake ukapata.
-Usijisahau kwamba wewe ni mwenye haki, Palilia haki yako mbele za MUNGU siku
zote. BWANA YESU asifiwe. Usikubali kulea tatizo ndani ya moyo wako.
Usilidharau tatizo lako kwamba ni dogo sana bali shughulika nalo hata kama ni
dogo sana. Ndugu yangu uliyekombolewa kwa damu ya YESU KRISTO, Baada ya
kukombloewa ulitakaswa na kupewa haki ya MUNGU katika KRISTO. Lakini wateule
wengi wana UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIROHO. -Haki yako idai huku ukiwa na sababu
kabisa kwamba haki yako ni halali kwako. -Watu wengi huona tu vinavyoonekana
lakini visivyoonekana ni vibaya zaidi, visivyoonekana ni mambo mabaya
unayokusudia moyoni mwako. Isaya 43:25-26 (Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye
makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.
Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako. ). Je
unaijua kesho yako katika MUNGU ikoje? Mambo mengine tunapanga sisi lakini
tambua kwamba mengine MUNGU ndiye anapanga, lakini MUNGU hakuwazii mabaya hata
siku moja bali yeye anakuwazia mema tu. Yeremia 29:11( Maana nayajua mawazo
ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa
ninyi tumaini siku zenu za mwisho. ). Palilia maisha yako ya kiroho. Palilia
safari yako ya mbinguni. Mfuate ROHO wa MUNGU siku zote za maisha yako. Luka
18:1(Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba MUNGU sikuzote, wala
wasikate tamaa. ) Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena
siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio
kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza
kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu
ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko
KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana . Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula Maisha
ya Ushindi Ministry. 0714252292
No comments:
Post a Comment