Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe 1.
Utangulizi Maandiko ya Msingi: Zaburi 18: 1-50, Waamuzi 6:1-40, Kipindi ambacho
Taifa la Israel walipokuwa watumwa wa wamidian, watu walikuwa wanaonewa sana na
kunyang’anywa mali zao hata mazao yao yalikuwa yakiharibiwa. Hivyo Gidion
alikuwa amejificha kwenye mwamba akipepeta ngano ndipo malaika akamwita ewe
shujaa Gidion,,lakini Gidion alikataa kuitwa shujaa kwa maaana alikuwa
hajiamini. Lakini malaika akamhakikishia kuwa yeye ni shujaa ila ile madhabahu
ya Baali aliyokuwa nayo baba yake ndiyo iliyokuwa inamshikilia hata asijitambue
kuwa ni shujaa. Hii inatufundisha kuwa kuna madhabahu mahali ambayo inakuzuia
wewe usifanikiwe kama Mungu alivyokusudia kwako. Kwenye madhabahu ile ya
nyumbani kwao Gidion kulikuwapo na ashera pia, ashera ni mti uliopandwa kwa
ajili ya kusimamia kitu fulani , kwa mfano mti unaweza kupandwa kwa jina la mtu
na ule mti ukistawi ndipo mtu Yule anapata matatizo mfano ugonjwa ndiyo maana
kuna mtu anakuwa mgonjwa wakati wa masika hii ni kwa sababu ya ule mti unakuwa
umenawili kwa mvua. Kuna mtu yuko mahali hapa na watu wasiompenda wamempandia
mti eidha wa balaa, magonjwa, umasikini, kukataliwa, kuachwa na kadhalika,
lakini leo tunatuma radi na kulipua maashera yote kwa jina la Yesu. Kwa hiyo
Gidion akaambiwa na bwana wewe ni shujaa unatakiwa kwenda kupigana vita ila
kwanza bomoa madhabahu iliyo kwenye mji huu inayofanya watu kuwa waoga. Na sisi
leo watu wa Ufufuo na Uzima tunaenda kila mahali ilipo madhabahu
inayolishikilia Taifa letu na tunaibomoa kwa jina la Yesu. Leo lazima watu wote
waliolazwa kwenye madhabahu ya nchi hii watatoka na kuelekea katika hatima zao
na mafanikio yao kwa jina la Yesu. Gidion baada ya kuibomoa madhabahu ya Baali
watu wa mji walimtafuta ili wamwuue lakini baba yake Gidion (Yoashi) akasema
mwacheni baali ajitetee mwenyewe kwa kubomolewa madhabahu yake, kwa hiyo
nakutangazia hata wewe leo hakuna dhara hata moja litakalokupata kwa kuzibomoa
madhabahu za wachawi . 2.0 MADHABAHU NDANI YA BIBLIA Mwanzo 8:20, Nuhu
alipotoka kwenye safina akamjengea Mungu madhabahu, Hii inaonyesha kuwa kila
madhabahu lazima iwe na tukio inaloliwakilisha, kwa mfano kuna madhabahu za
utawala, kwa hiyo huwezi kumwondoa mtawala aliye na madhabahu imara mpaka
uibomoe ile madhabahu ndipo uguse utawala wake. Mwanzo 12:7, Ibrahim alipoongea
na bwana kwamba nchi ile amepewa ndipo alipojenga madhabahu mahali pale ili
isimamie umiliki wake aliopewa kwenye ile nchi, ndiyo maana hata sasa hakuna
mtu anayeweza kuwanyang’anya wa Israel nchi yao ingawa mataifa mengi wamejaribu
kuwaondoa lakini wameshindwa. Mwanzo 12:8, 13:14, Utaona watu kwenye biblia
walikuwa wakijenga madhabahu mahali ili isimamie jambo fulani. Madhabahu ni
mahali ambapo wachawi na waganga wa kienyeji wanakusanyikia , wanapokuwa mahali
pale wanatoa kafara za damu na wanakuja na mashitaka ya kuwashitaki watu na
wananza kujadili. Kwa hiyo mchawi mmoja anapeleka shitaka la kumshitaki mtu kwa
mfano atasema simpendi fulani kwa sababu analinga eti anahela ,au ana watoto
wasomi au anapendwa sana na watu hivyo nataka tumkomeshe. Kwa hiyo wachawi
wanasema sawa tutamkomesha na ndipo wanapoanza kumtumia mtu mashetani ya
kumharibia maisha yake. Lakini leo nakutangazia kuwa madhabahu zote zilizotesa
maisha yako lazima zibomolewe kwa jina la Yesu. Ninayo ndoto na ndoto yangu ni
kuwa Falme za dunia zimekuwa Falme za mwanakondoo na hii imeishakuwa kwa maana
madhabahu za kichawi zilizozuia injili ya Yesu zitabomolewa zote kwa jina la
Yesu. Mchawi anapenda kumshambulia na kumwuua mtu wa karibu yake kwa mfano
kaka, dada, mama, baba nakadhalika. Kwa mfano mtu anataka dada fulani asiolewe
kabisa, anapeleka jina lake kwenye madhabahu na kumwaga kafara, kwa hiyo
kuanzia pale yule dada hawezi kuolewa kabisa kwa maana madhabahu inakuwa
inaongea fulani asiolewe, asiolewe. Mwingine anaweza kuwekwa kwenye madhabahu
ya uoga, kwa hiyo hawezi kufanya lolote kwa kuogopa eidha hasara kama ni
biashara, ajali kama ni safari, kuachwa kama ni ndoa nakadhalika. Madhabahu
inaweza kuwa kakiwanja fulani ambapo wachawi wanakutanikia na kutoa kafara za
damu kwa miungu wao. Mtu anaposhitakiwa na jina lake kutajwa mahali pale ndipo
mashetani yanaanza kumwandama na kumharibia mambo yake, kwa hiyo mtu yule
hawezi kufanikiwa hata afanyeje mpaka atakapoibomoa ile madhabahu. Madhabahu
zinapobomolewa watu wanaachiliwa kwa hiyo wachawi na waganga wa kienyeji
wanapata hasara, ndiyo maana Gidion alitafutwa auawe kwa kuibomoa madhabahu ya
baali iliyokuwa nyumbani kwa baba yake Yoashi. Leo tutabomoa madhabahu
iliyokutesa na kuwalaza kwenye hiyo madhabahu wale waliokuwa wamekulaza kwa
jina la Yesu. Madhabahu /kiwanja cha wachawi huwezi kukiona kwa macho lakini
kipo na wachawi wanakutana pale kila usiku na kuwashitaki watu. Ndiyo maana
utaona watu wengi wana matatizo yasiyoisha, kwa mfano kuna mtu amelazwa kwenye
madhabahu ya kuachwa kwenye ndoa kwa hiyo utamwona mama ameshaolewa na wanaume
watatu nakuachwa na wote bila sababu ya msingi. Mungu anapotaka kumwinua mtu
anaruhusu apitie mambo magumu sana kila upande na asione msaada. Ndipo sasa mtu
anapoona hana msaada anakumbuka kumlilia Mungu. Kwa mfano Israel walipokuwa na
njaa kali sana mpaka watu wamefikia hatua ya kula watoto wao, ndipo Mfalme
akasema mwambie nabii Elisha kesho saa saba atakatwa kichwa asipotabiri kwa
habari ya njaa kwenye taifa la Israel. Baada ya kutishwa ndipo nabii Elisha
alitoa unabii kwamba kesho chakula kitapatikana tena kwa bei nafuu sana kuliko
hata kabla ya njaa kutokeaa na kesho yake yakatokea kama vile Elisha
alivyosema. Hii inafundisha kuwa mtu unapopata matatizo usianze kulia wala
kuwalaumu watu bali wakati huo ni wakatiwa kuutafuta uso wa Mungu ili upate
jibu la kukutoa mahali pale. Usifikiri magumu yanayokupata Mungu amekuacha siyo
ni kwamba Mungu anataka uanze kumlilia na kumtafuta yeye kwa moyo wako wote kwa
maana aliona umeanza kwenda mbali naye. Kwa hiyo kuna madhabahu ambayo inaweza
kuwa imemshikilia mtu mfano mtu anaweza kuwa amelazwa kwenye madhabahu ya
umasikini hata akisoma na kusafiri nchi zote duniani hawezi kufanikiwa. Kwa
hiyo ili mtu huyo afanikiwa lazima aibomoea ile madhabahu. Leo kila mtu ataomba
kulingana na udhaifu alio nao kwenye maisha yake kwa mfano mtu mwenye hofu
ataomba akisema kwa jina la Yesu naibomoa madhabahu ya hofu iliyonishikilia na
kuiharibu kafara waliyoitoa kwenye hiyo madhabahu. Kwa jina la Yesu leo naamuka
na kuondoka kwenye madhabhu walioyonilaza kwa jina la Yesu. Na mtu yeyote
aliyepeleka jina langu kwenye madhabahu hiyo namponda kwa jina la Yesu. Wakati
mwingine madhabahu inaweza kuwa siyo kiwanja bali inakuwa kwenye kitu chochote
kile, kwa mfano dada mmoja alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni ya tajiri, siku
moja yule dada akaingia kwenye ofisi ya boss wake na kuona chupa ndogo lakini
ndani ya ile chupa yumo yule dada akiwa hai. Hii inatufundisha kuwa yule dada
alikuwa amelazwa kwenye madhabahu ya yule tajiri , kwa hiyo mafanikio aliyonayo
yule tajiri ni kupitia nyota ya yule dada. 3.0 MAMLAKA TULIYOPEWA NA BWANA WETU
YESU KRISTO Mathayo 10:1, kwa hiyo watu wa Mungu tumepewa mamlaka ya kutamka na
ikawa na leo tunaenda kuzibomoa madhabahu zote kwa jina la Yesu. Mambo hapa
dunia hayatokei yenyewe ila kuna kitu kinafanywa ili yatokee. Na nguvu ya
kufanya mambo yatokee ni uwezo wa mtu wa Rohoni alionao ndiyo unaleta matokeo
mazuri ya mwilini. Kwenye ulimwengu wa Roho unapotamka kwamba navunja madhabahu
iliyonishikilia mahali popote itakuwa kama utakanyotamka. 4.0 HITIMISHO 4.1 MAOMBI
Kwa damu ya mwanakondoo naibomoa madhabahu ya wachawi kwa jina la Yesu, mahali
popote walipotaja jina langu napaharibu kwa jina la Yesu, Naibomoa hali ya kuwa
kichaa, naibomoa madhabahu ya wendawazimu,naibomoa madhabahu ya mikosi kwa jina
la Yesu. Mtu yeyote aliyenilaza kwenye madhabahu yake ya utawala leo naondoka
na nakataa kubaki pale kwa jina la Yesu na nyota yangu naimuru ianze kung’aa.
Nakataa watoto wangu , kazi yangu, ukoo wangu kuwekwa kwenye madhabahu ya
wachawi kwa jina la Yesu. Naibomoa madhabahu ya kifo, umasikini,uoga na mikosi
kwa jina la Yesu. Imeandikwa Gidion aliwapeleka watumishi wake kumi wakaibomoa
madhabahu ya baali, na sisi watumishi wa Mungu leo tunazibomoa madhabahu zote
zilizoshikilia taifa letu na watu kwa jina la Yesu. Imeandikwa bomoeni bomoeni
hadi msingini, leo nabomoa madhabahu zote, madhabahu ya dhiki, magonjwa,
umasikini kwa jina la Yesu. Nabomoa madhabahu ya shaba, udongo, chuma ,mti kwa
jina la Yesu. Nakataa kushikiliwa kwa jina la Yesu, mtu yeyote anayenicontrol
kupitia madhabahu yoyote leo nakaataa kwa jina la Yesu. Madhabahu ya mabaya
iliyoimarishwa naivunja kwa jina la Yesu, mabaya hayatanipata mimi. Naamuru
mizimu, majini, majoka anza kuondoka kwa maana madhabahu zenu zimebomolewa kwa
jina la Yesu. Imeandikwa bwana amenifunga mshipi wa vita, leo nafanya vita na
kuziteketeza madhabahu zote na nawachinja makuhani wote wa hizo madhabahu.
Naivunja madhabahu inayoninyima promosheni,inayonizuia nisisafari, inayonizuia
nizipate pesa kwa jina la Yesu,. Na kuhani yeyote aliyenipeleka kwenye hizo
madhabahu leo namchinja . Imeandikwa bomoeni bomoeni hadi msingi leo naenda
kubomoa madhabahu za njia panda, porini, bahari . Nainyamazisha damu
iliyomwagwa kwenye madhabahu za wachawi kwa damu ya Yesu. Ninaamuru kuanzia
sasa kila madhabahu inayonena nainyamazisha kwa jina la Yesu. Kila madhabahu
iliyojengwa kwenye nchi ya Tanzania ili kukamata akili na nia za watanzania leo
nakupasua vipanda vipande kwa jina la Yesu. Naamru na roho zote zilizolazwa
kwenye madhabahu zianzae kuamka kwa jina la Yesu. Nakata kamba zote
zinazounganisha watu na madhabahu za wachawi kwa jina la Yesu. Nakata ashera
zote zilizopandwa kwa majina ya watu kwa jina la Yesu. Nazilaani ashera zote na
kuanzia sasa zianze kukauka kwa jinala Yesu. Nawateka nyara wasimamizi na
makuhani wa madhabahu nawachinja kwa jina la Yesu. Ewe Mungu wa madhabahu
nakukamata na kukuteketeza kabisa na enzi yako yote kwa jina la Yesu. Leo
naamuru mioyo, nafsi, akili na vyote vilivyoshikiliwa kuachiliwa kwa jina la
Yesu. Nauzima moto uliwashwa kwenye madhabahu ya wachawi ili watu wapate
magonjwa, kichaa, umasikini , balaa na mikosi kwa jina la Yesu. Naibomoa
madhabahu iliyojengwa kwenye kichwa, tumbo, kifua kwa jina la Yesu. Naibomoa
madhabahu iliyohai na inayotembea kwa jina la Yesu. Ufunuo 6:9, kuna roho za
watu zinaweza kuwa zimewekwa chini ya madhabahu. Hata wewe leo unaweza kuwa
hapa lakini roho yako imelazwa kwenye madhabahu, sema leo naivunja madhabahu
iliyonilaza na toka kwa jina la Yesu. Wachawi wa familia wanaweza kumwuuza mtu
na kumpeleka alazwe kwenye madhabahu. Leo naiteketeza hati ya makubaliano yao
ambayo imewekwa kwa jina la Yesu, hati iliyonifanya niuzwe na nibaki
madhabahuni leo naichana na kuiteketeza kabisa kwa kwa jina la Yesu. Ufufuo na
Uzima,Tanganyika parkers Kawe
No comments:
Post a Comment