MUNGU ALITUVISHA
HAKUTUACHA TUWE UCHI.
Na mtumishi Lusajo Brown
Somo hili limekuja ghafla moyoni mwangu wakati nilipokuwa nikiwaza na
kuwazua kuhusu maisha ya wanadamu wa kizazi tulichonacho.
Ni Mara nyingi nakutana na wadada wakiwa wamevaa nguo wakati sehemu
kubwa ya maziwa yao yakiwa nje na wala hana wasiwasi anatembea
barabarani na mwingine kavaa gauni ama sketi ndefu inafika miguuni
lakini nguo za ndani zinaonekana na wengine hadi maumbile yao
yanaonekana maana hawajavaa chochote ndani ya nguo hiyo na wengine
wamevaa nguo ndefu lakini imechanwa mpaka mapajani kwa hiyo yanaonekana,
mifano ni mingi nadhani wengi wanaojua maungo ya siri ya mwanamke na
hata mwanaume atakuwa ananielewa kwa mfano wanaume nao hupenda kutembea
vifua wazi ama kuvaa vibukta vifupi na kutembea barabarani bila wasiwasi
cha msingi cha kuelewa ni kwamba hakuna mahali katika Biblia
panapomruhu mtu wa jinsia yoyote kuvaa nusu uchi ama uchi kabisa.
Tusome pamoja.
Mwanzo 3.
21 BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.
Mungu akawavika wanadamu wa kwanza ambao ndiyo asili yetu.
**Kwanini basi aliwavika wanadamu, na asiwavike wanyama wengine?
> Wanadamu ni tofauti na wanyama maana waliumbwa kwa mfano wa Mungu.
Mwanzo 1:27 alifumbuliwa macho...yaani walipewa kujitambua. Walipewa
ufahamu.
Mwanzo 3
7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona
majani ya mtini, wakajifanyia nguo.
Swali la kujiuliza, Je? Ufahamu huo dunia umetoweka... Kujitambua katika
kizazi hiki kumeondoka?
Kiasi cha wanadamu kutamani maisha ya wanyamaaa...
Ooooooooooh
Mungu tusaidieeee
Mwanadamu anataka atembee kama mbuzi, kama mbwa barabarani.
Aibu hii imetoweka ndani yetu...
Mwanzo 3
9 BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?
10 Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni
uchi; nikajificha.
11 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe
matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?
Mti ule ulitupa kujitambua, uliweka aibu ndani yetu ndiyo maana kwa
asili hiyo tunaona hata juu ya watoto wetu kwamba kuna wakati hata
wakiwa uchi huja tu hata mbelea za wageni bila wasiwasi lakini kila
ufahamu unapojuja utaona wakiwa uchi hujificha wenyewe kama walivyofanya
Adamu na mkewe baada ya kuisikia sauti ya Mungu.
Je wewe baada ya kuisikia sauti ya Mungu umechukua hatua gani? Je
utaendelea kutembea barabarani kama afanyavyo mbwa?
Na wengine huendelea kujifariji kwa maneno ya uongo uleule wa shetani
kwa kuvaa mavazi wasiyositahiri na kusema wanaenda na wakati.
Wakati Mungu amekataa waziwazi.
Kumbukumbu 22
5 Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae
mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa
BWANA, Mungu wako.
Mwanamke kwani ni lazima kwako kuvaa suruali...acha visingizio eti
kwamba kuna za kike lakini je asili ya mavazi hayo ni nini au unafikiri
ni kwanini Mungu alipenda uvae nguo ambayo iko wazi ama pana chini.....
Huo wote ni mchezo wa shetani....
Maana shetani tangu mwanzo aliuona upendo wa Mungu kwetu kiasi cha
kutuumba kwa mfano wake hivyo Mara zote shetani hutengeneza mbinu
kuhakikisha anatukosanisha na Mungu. Maana shetani ni malaika aliye asi
hivyo siri hii anaijua.
Shituka sasa mwanadamu ili turudie Edeni, jua baada ya kuifuta Edeni ya
Duniani, Mungu ameandaa mji mwingine mbinguni ambako Yesu ameenda
kutuandalia makao ili alipo yeye na sisi tuwepo.
Sijui nitumie maneno gani.
Lakini Mungu akusaidie.
Kama bado hujaokoka, wakati ndiyo sasa, maana baada ya kufa ni hukumu.
Kumbuka Mungu alishona mavazi ya ngozi akakuvisha.
Mungu akubariki wewe uliyechukua hatua baada ya kusoma ujumbe huu.
Amen
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
No comments:
Post a Comment