Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe I.
UTANGULIZI. Danieli 1:1-21 Kweye biblia neno chakula limeandikwa mara 185 na
neno usile limeandikwa mara 15 na shetani hana nguvu juu ya watu wa Mungu mpaka
anapopata nafasi na shetani amepata nafasi kubwa sana kwenye chakula kwa
kuwaangamiza watu na kuna aina mbili za chakula chakula cha kiroho na chakula
cha kimwili 1wakorintho10: 1 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya
kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; 2
wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; 3 wote wakala
chakula kile kile cha roho; 4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa
maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. 5
Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa
jangwani. 6 Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa
kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani. 7 Wala msiwe waabudu sanamu, kama
wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa,
kisha wakasimama wacheze. 8 Wala msifanye uasherati, kama wengine wao
walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu. 9 Wala
tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka. 10
Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakaharibiwa na
mharabu. 11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili
kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. 12 Kwa hiyo anayejidhania
kuwa amesimama na aangalie asianguke. 13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa
lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe
kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea,
ili mweze kustahimili. 14 Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya
sanamu. 15 Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo. 16
Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate
ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? 17 Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi
tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate
mmoja. 18 Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale
wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu? 19 Basi niseme nini? Ya
kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni
kitu? 20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala
si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea
kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. 21 Hamwezi kushirikiana katika meza
ya Bwana na katika meza ya mashetani. Biblia ukisema chakula cha kiroho unaweza
kutafasiri mambo mawili yani chakula cha rohoni yani chakula cha kiroho. Lakini
ni chakula gani kimeitwa chakula cha kiroho kulikuwa na vipande vya mikate
vidogovidogo walikula chakula hichohicho tangu waanze safari mpaka mwisho wa
safari kwamaana kwamba kulikuwa na nguvu kwenye chakula hicho kunakuwa na nguvu
ndani ya chakula hichi kinaonekana cha kimwili ni cha kawaida lakini ndaniyake
kuna nguvu za Mungu na anayekula anaonekana ana kula chakula chenye
virutubisho. II. SOMO. Ndani ya chakula kunaweza kuwa na mauti na uzima. Baada
ya Israeli kuvamiwa wana wa Israeli walipelekwa mpaka nchi ya Babeli (Iraq)
utumwani. Walipofika babeli walilazimishwa kula chakula ambacho kimetolewa
sadaka kwa miungu na akinadanieli wakaambiwa wabadilishe majina yao na kabla
mfalme hajala kile chakula cha mfalme kinachukuliwa alafu kinaombewa kitu
Fulani kwamba mtu atakapokula awe mtu wa aina Fulani, Yesu alisema yeye alayee
chakula changu anauzima alafu akasema Baba zenu walikula chakula wakafa lakini
mimi ninachakula cha uzima sasa wewe unapokaribishwa kwenye chakula ambacho
kimenuiziwa mambo ya kichawi mambo ya kishetani unapatwa na kansa, magonjwa na
matatizo na leo ni mwisho. Yohana6: 46 Wale watumishi wakajibu. Hajanena kamwe
mtu ye yote kama huyu anavyonena. 47 Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! Ninyi
nanyi mmedanganyika? 48 Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo?
49 Lakini makutano hawa wasioifahamu torati wamelaaniwa. 50 Akawaambia
Nikodemo, (naye ni yule aliyemwendea zamani, maana ni mmoja wao), 51 Je! Torati
yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza, na kujua atendavyo? 52 Wakajibu,
wakamwambia, Je! Wewe nawe umetoka Galilaya! Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka
Galilaya hakutokea nabii. Hata alipokuwa na wanafunzi wake aliwaonyesha kwa
kuchukua mkate na kuwaambia yeye aulaye mwili wangu atakuwa na uzima wa milele
na kwasababu hiyo ule mkate uliingia nguvu ya Yesu kristo unaingia ndani yake.
Shetani ni malaika wa ngazi ya kerubi. Yuda1: 6 Na malaika wasioilinda enzi yao
wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya
milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu., Ufunuo12: 7 Kulikuwa na vita
mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana
nao pamoja na malaika zake; malaika wanasifa mojawapo ya kugeuza maumbo.
Ndiomaana Ibrahumu aliwapokea malaika wenye maumbo ya watu na mavumbi na
akawaandalia chakula wale mabwana wakakaa na kusubiria chakula wakala, sio kila
mwenye mavumbi miguuni ni mtu, sio kila anayepiga stori ni mtu, ndiomaana
kwenye chakula unaweza kula chakula kilicho nuiziwa unakula balaa, magonjwa,
ajali, mauti, bila ya kujua. Hesabu25: 2 kwa kuwa waliwaalika hao watu waende
sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu
hiyo miungu yao. 3 Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana
zikawaka juu ya Israeli. 4 Kisha Bwana akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa
hao watu, ukamtungikie Bwana watu hao mbele ya jua, ili kwamba hizo hasira kali
za Bwana ziwaondokee Israeli. 5 Basi Musa akawaambia waamuzi wa Israeli, Waueni
kila mtu watu wake waliojiungamanisha na Baal-peori. Chakula mtu anakitoa
sadaka kwa mashetani kinanuiziwa mfano kwenye mila wanachukua pombe na mtama
wanakunywa wanaongea maneno maanayake wanatoa sadaka na mashetani, majini,
mapepo ugali, pilao, au chakula chochote na unapokula wanaingia mwilini na
kufanya kazi ya uharibifu na wewe na hayo mashetani mnakuwa kitu kimoja. Kuna
watu wengi wagonjwa kwasababu ya chakula na Matendo ya mitume15:20 bali
tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama
zilizosongolewa, na damu. 1Wakorintho10: 20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo
sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana
na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. 21
Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. 22 Au
twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye? 23 Vitu vyote ni halali; bali
si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo.
1Wafalme19:1 Basi, Ahabu akamwambia Yezebeli habari ya mambo yote aliyoyafanya
Eliya, na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga. 2 Ndipo Yezebeli
akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi,
nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa
hao. 3 Naye alipoona hayo, aliondoka, akaenda aihifadhi roho yake, akafika
Beer-sheba, mji wa Yuda, akamwacha mtumishi wake huko. 4 Lakini yeye mwenyewe
akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi chini ya mretemu.
Akajiombea roho yake afe, akasema, Yatosha; sasa, Ee Bwana, uiondoe roho yangu;
kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu. 5 Naye akajinyosha akalala chini ya
mretemu; na tazama, malaika akamgusa, akamwambia, Inuka, ule. 6 Akatazama,
kumbe! Pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake.
Akala, akanywa, akajinyosha tena. 7 Malaika wa Bwana akamwendea mara ya pili,
akamgusa, akasema, Inuka, ule; maana safari hii ni kubwa mno kwako. 8 Akainuka,
akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arobaini mchana na
usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu. Kumbe unaweza ukapewa chakula cha
kishetani ukatembea kwenye balaa kwa chakula hicho mpaka ukaingia mautini na
unatakiwa uangalie pale unapokaribishwa chakula kunauzima humo. Lazima ujue
mitego ya mwindaji kwingine umefanikiwa lakini anaweza kukukamata kwenye
chakula na unatakiwa useme “Baba Mungu ninaweka Baraka kwenye chakula hiki kwa
jina la Yesu”. Kunaweza kuwa na mauti na mauti sio tukio mauti ni roho ni jini
kumbuka wana wa manabii waliona roho ya mauti kwenye sufuria. Mtu anaweza
akanuizia jambo Fulani kwenye chakula. Kama Mungu alivyo na watu wake na
shetani naye ana watumishi wake. Wakiona imeshindikana kukuletea chakula
wanaanza kukuletea ndotoni, ndiomaana unakuta mtu anatafuna akiwa amelala.
Tulipookolewa tunalindwa na Mungu kwa njia ya Imani na ndio maana unapotaka
kulala lazima uombe na sio useme Bwana Yesu shuka utulinde hapa! Tunaotenda
kazi ni sisi tena kwa ujasiri unawaamuru malaika wakulinde. “Kwa jina la Yesu
ikiwa tatizo langu lilianza kwenye chakula nilichopewa kuanzia leo ninakataa
kwa jina la Yesu” ndoto ni bayana hakuna aliyeota hakikutokea kina
Ebimeleki,yusufu utawala, farao njaa, nebkandneza, askari wa jeshi la midiani
kwa mikate iliyoanguka toka mbinguni, hakuna aliyeota ndoto haikutokea. Kama
uko imara ndotoni unaota umekaribishwa lakini wewe huli maana yakee uko imara.
Wanaolishwa chakula ndotoni kama uko juu unashushwa chini, kama unakazi
unaipoteza kazi hiyo, kushindwa kuomba. Kunawatu wengi wamelishwa chakula
nyumbani kwa mtu na wameharibikiwa maisha yao ”kwa jina la Yesu kuanzia leo
magonjwa niliyoyapata kwa kulishwa chakula ndoton ninayakataa kwa jina la Yesu
mahala popote nilipokula chakula cha kichawi kuanzia leo enyi mashetani
mlioniwekea kutokuolewa kutokufanikiwa kuanzia leo ninawafyeka kwa jina la Yesu
navunja maagano yaliyokuwa ndani ya chakula ninayavunja kwa jina la Yesu
maagano ya mauti, maagano ya kifo ninayavunja kwa jina Yesu ninaagiza kuanzia
sasa majini, majoka , mizimu walionuiziwa kwenyee chakula cha ndotoni, kwenye
chakula cha mwilini kuazia leo ninakataaa kwa jina la Yesu”.( ukitaka kutatua
tatizo unatakiwa ujue chanzo cha tatizo”) Wengine kwa njia ya chakula wanaweza
kuchukua nyota yako wananuizia kabisa na hakuna kinachotokea chenyewe vitu
vinatengenezwa ndio maana duniani Kuna watu wa aina tatu. 1. Wale wanaoona
matukio yanatokea tu lakini hawajuwi kinachoendelea. 2. Wale wanaojua
kinachoendelea; wakiona nchi wanajua kinachoendelea wakiona mtu kafa wanajua
kinachoendelea 3. Watu wanaotengeneza mambo yatokee wakitaka upatwe ugonjwa
unapatwa na ugonjwa. Tukidili na chanzo cha tatizo tunalimaliza tatizo, kuna
mamlaka ya rohoni inayotegemewa kusimamisha mambo Fulani. Maisha ya mtu
hujulikana kabla hayajaanza; Yeremia anasema Kabla sijakuumba katika tumbo
nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa
mataifa. Inawezekana wamekupotezea miaka mingi lakini Mungu anaweza
kukurudishia vyote vilivyopotea, Mungu ni Mungu wa nafasi ya pili na usiangalie
vile ulivyo Biblia inasema amelaaniwa yeye amtegemeaye mwanadamu kwa jambo
lolote. Baraka ndani ya chakula na laana ndani ya chakula, kabla hujazaliwa
Baraka zako zinaonekana ukiwa tumboni mwa mama yako. Kuna wakati mwingine mtu
huwa hapendi lakini hubalansi kwasababu ya urafiki, kuna mambo unakula leo
halafu madhara yanaanza mwaka kesho. Haung’ai kwasababu unavyoonekana kwa nje
hapana bali kuna kitu kimewekwa ndani yako na Mungu na wachawi hukiona na
kukichukua na wewe unadhani unafanyiwa fitina kumbe ulipewa chakula
kilichonuiziwa. Kilichowekwa ndani yako kinakupigisha hatua kwa elimu na
kisipokuwepo unakuta unasoma lakini hauwezi kufanikiwa kumbe ni chakula. “Kwa
jina la Yesu ninajikinga na chakula au vinywaji au kitu chochotee kilichotolewa
sadaka kwa mashetani na mtu yeyote aliyetoa sadaka ninamteketeza kwa jina la
Yesu chochote alichonipa mtu ndugu rafiki au mtu yeyote bila kujua nikala au
nikanywa kuanzia leo yamrudie yeye mwenyewe kwa jina la Yesu” unamatatizo na
haujui matatizo hayo yanatokea wapi na kuwa wa kwanza darasani sio kuwa na
maisha mazuri lakini Mungu ameweka kitu ndani ya mtu nyota uwezo karama
imewekwa ndani ya mtu na elimu inamsaidia mtu huyo. Kila chakula unachokula
lazima kiwe kimetolewa sadaka mahali Fulani na ndio maana watu wa Mungu
wanapotaka kula wanakiombea “kwa jina la Yesu ninawashinda wote walioandaa
chakula wiki hii kwenye ndoto, kwenye sherehe nawashinda kwa jina la Yesu”
Unapokaribishwa chakula lazima uangalie unaweza kula kilichonuiziwa na shida
watu wamezoea kuombewa, unatakiwa ujifunze kupigana wewe mwenyewe unapiganaje
unapigana kwa jina la Yesu”kwa jina la Yesu kila chakula kilichoandaliwa
kichukue nyota naamuru roho yangu ikatae kwa jina la Yesu. Kwa jina la Yesu
kila aliyeandaa chakula cha mauti, kinywaji cha kifo namrudishia yeyee kwa jina
la Yesu aliye andaa kwenye ndoto au mahala popote ninakataa kwa jina la Yesu”
kila unachosema kinakuwa. Kwanini ninasisitiza kuomba mathayo10: 8 Pozeni
wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni
bure. Kila mtu aliyempokea Yesu anauwezo 1 Akawaita wanafunzi wake kumi na
wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na
udhaifu wa kila aina. Marko7:6 luka 10:19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga
nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.
Kwahiyo usiseme niombeeni unatakiwa uvunje mwenyewe kama unamjua mchawi
unamtaja na jina Mathayo18: 18 Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani
yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa
yamefunguliwa mbinguni. Vita vya rohoni ni kwamba wewe unaomba ukitaja maneno
na utakuwa vile unavyoamini. Sisi mbele za Mungu ni watoto wa Mungu na Mungu
hutenda sawa na vile vile unavyoamini, ukiamini nikimfunga shetani anafungika
na inakuwa hivyo hivyo ulivyoamini. III. UKIRI Baba wa mbinguni nimeisikia
sauti yako na ninaomba nguvu ya uweza kushindana na wakala wote wa shetani na
kila mtu aliye nihusisha kwa jambo lolote la kuweza kunisababishia uharibifu
ndani yangu leo ninaomba asipate nguvu juu yangu na kwasababu hiyo ninapokea
nguvu na kujitakasa. IV. MAOMBI Katika jina la Yesu kristo mwana wa Mungu aliye
hai ninavunja mashetani yote yaliyoingizwa kwenye familia yangu kwa njia ya
chakula kwa jina la Yesu. Ninasambaratisha kuanzia sasa magonjwa yaliyopandwa
kwa njia ya chakula ninayaharibu na kuyaangamiza kwa jina la Yesu, kila kufeli,
kuanguka kulikosababishwa kwa njia ya chakula ninasimama kinyume nacho kwa damu
ya mwana Kondoo, kila kinywaji nilichokinywa kila kushindwa kulikosababishwa
kwasababu ya chakula ninasambaratisha kwa jina Yesu, ninaharibu wasimamizi wa
chakula mlioungamanishwa na chakula kwa damu ya mwanakondoo, ninafungua
vingufungo vyote vilivyofungwa na wakala wa shetani kwenyee familia yangu na
maisha yangu kwa njia ya chakula ninabomoa kwa damu ya mwanakondo katika jina
la Yesu, mauti iliyoingia kwa njia ya chakula ninaiharibu kwa jinala laYesu,
ninaharibu udhaifu wowote ulionuiziwa kwenye chakula juu yangu kwa damu ya
mwana kondoo, “vita sio vyangu vita ni vya Bwana” ninaharibu kila chanzo cha
magonjwa, mikosi, kukataliwa, ninafungua kamba zote katika jina la Yesu. Kwa
jina la Yesu kila atakaye niletea zawadi au chakula kwa njia ya siri naiamuru
laana ile imrudie yeye kwa jina la Yesu lakini mimi sitalogwa kwa jina la Yesu.
AMEN. Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe
CHAKULA CHA KICHAWI
Na Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima.
Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe I.
UTANGULIZI.
Danieli 1:1-21
Kweye biblia neno chakula limeandikwa mara 185 na neno usile
limeandikwa mara 15 na shetani hana nguvu juu ya watu wa Mungu mpaka
anapopata nafasi na shetani amepata nafasi kubwa sana kwenye chakula kwa
kuwaangamiza watu na kuna aina mbili za chakula chakula cha kiroho na
chakula cha kimwili 1wakorintho10: 1 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi
mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote
wakapita kati ya bahari; 2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na
katika bahari; 3 wote wakala chakula kile kile cha roho; 4 wote
wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa
roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. 5 Lakini wengi sana
katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani. 6 Basi
mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani
mabaya, kama wale nao walivyotamani. 7 Wala msiwe waabudu sanamu, kama
wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na
kunywa, kisha wakasimama wacheze. 8 Wala msifanye uasherati, kama
wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu
elfu. 9 Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu,
wakaharibiwa na nyoka. 10 Wala msinung'unike, kama wengine wao
walivyonung'unika, wakaharibiwa na mharabu. 11 Basi mambo hayo
yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi,
tuliofikiliwa na miisho ya zamani. 12 Kwa hiyo anayejidhania kuwa
amesimama na aangalie asianguke. 13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa
lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha
mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na
mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. 14 Kwa ajili ya hayo, wapenzi
wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. 15 Nasema kama na watu wenye akili;
lifikirini ninyi ninenalo. 16 Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je!
Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili
wa Kristo? 17 Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja;
kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja. 18 Waangalieni
hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je!
Hawana shirika na madhabahu? 19 Basi niseme nini? Ya kwamba kile
kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu? 20
Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala
si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi
kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. 21 Hamwezi
kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. Biblia
ukisema chakula cha kiroho unaweza kutafasiri mambo mawili yani chakula
cha rohoni yani chakula cha kiroho. Lakini ni chakula gani kimeitwa
chakula cha kiroho kulikuwa na vipande vya mikate vidogovidogo walikula
chakula hichohicho tangu waanze safari mpaka mwisho wa safari kwamaana
kwamba kulikuwa na nguvu kwenye chakula hicho kunakuwa na nguvu ndani ya
chakula hichi kinaonekana cha kimwili ni cha kawaida lakini ndaniyake
kuna nguvu za Mungu na anayekula anaonekana ana kula chakula chenye
virutubisho.
II. SOMO.
Ndani ya chakula kunaweza kuwa na mauti na uzima. Baada ya Israeli
kuvamiwa wana wa Israeli walipelekwa mpaka nchi ya Babeli (Iraq)
utumwani. Walipofika babeli walilazimishwa kula chakula ambacho
kimetolewa sadaka kwa miungu na akinadanieli wakaambiwa wabadilishe
majina yao na kabla mfalme hajala kile chakula cha mfalme kinachukuliwa
alafu kinaombewa kitu Fulani kwamba mtu atakapokula awe mtu wa aina
Fulani, Yesu alisema yeye alayee chakula changu anauzima alafu akasema
Baba zenu walikula chakula wakafa lakini mimi ninachakula cha uzima sasa
wewe unapokaribishwa kwenye chakula ambacho kimenuiziwa mambo ya
kichawi mambo ya kishetani unapatwa na kansa, magonjwa na matatizo na
leo ni mwisho.
Yohana6: 46 Wale watumishi wakajibu. Hajanena kamwe mtu ye yote kama
huyu anavyonena. 47 Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! Ninyi nanyi
mmedanganyika? 48 Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo?
49 Lakini makutano hawa wasioifahamu torati wamelaaniwa. 50 Akawaambia
Nikodemo, (naye ni yule aliyemwendea zamani, maana ni mmoja wao), 51 Je!
Torati yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza, na kujua atendavyo?
52 Wakajibu, wakamwambia, Je! Wewe nawe umetoka Galilaya! Tafuta,
ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii.
Hata alipokuwa na wanafunzi wake aliwaonyesha kwa kuchukua mkate na
kuwaambia yeye aulaye mwili wangu atakuwa na uzima wa milele na
kwasababu hiyo ule mkate uliingia nguvu ya Yesu kristo unaingia ndani
yake. Shetani ni malaika wa ngazi ya kerubi.
Yuda1: 6 Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha
makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya
giza kwa hukumu ya siku ile kuu., Ufunuo12: 7 Kulikuwa na vita mbinguni;
Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye
akapigana nao pamoja na malaika zake; malaika wanasifa mojawapo ya
kugeuza maumbo. Ndiomaana Ibrahumu aliwapokea malaika wenye maumbo ya
watu na mavumbi na akawaandalia chakula wale mabwana wakakaa na
kusubiria chakula wakala, sio kila mwenye mavumbi miguuni ni mtu, sio
kila anayepiga stori ni mtu, ndiomaana kwenye chakula unaweza kula
chakula kilicho nuiziwa unakula balaa, magonjwa, ajali, mauti, bila ya
kujua.
Hesabu25: 2 kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka
walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu
yao. 3 Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana
zikawaka juu ya Israeli. 4 Kisha Bwana akamwambia Musa, Watwae wakuu
wote wa hao watu, ukamtungikie Bwana watu hao mbele ya jua, ili kwamba
hizo hasira kali za Bwana ziwaondokee Israeli. 5 Basi Musa akawaambia
waamuzi wa Israeli, Waueni kila mtu watu wake waliojiungamanisha na
Baal-peori.
Chakula mtu anakitoa sadaka kwa mashetani kinanuiziwa mfano kwenye mila
wanachukua pombe na mtama wanakunywa wanaongea maneno maanayake wanatoa
sadaka na mashetani, majini, mapepo ugali, pilao, au chakula chochote na
unapokula wanaingia mwilini na kufanya kazi ya uharibifu na wewe na
hayo mashetani mnakuwa kitu kimoja.
Kuna watu wengi wagonjwa kwasababu ya chakula na Matendo ya mitume15:20
bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati,
na nyama zilizosongolewa, na damu.
1Wakorintho10: 20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa
mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na
mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.
21 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya
mashetani. 22 Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye? 23
Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali;
bali si vitu vyote vijengavyo.
1Wafalme19:1 Basi, Ahabu akamwambia Yezebeli habari ya mambo yote
aliyoyafanya Eliya, na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga. 2 Ndipo
Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na
kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya
mmojawapo wa hao. 3 Naye alipoona hayo, aliondoka, akaenda aihifadhi
roho yake, akafika Beer-sheba, mji wa Yuda, akamwacha mtumishi wake
huko. 4 Lakini yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku
moja, akaenda akaketi chini ya mretemu. Akajiombea roho yake afe,
akasema, Yatosha; sasa, Ee Bwana, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si
mwema kuliko baba zangu. 5 Naye akajinyosha akalala chini ya mretemu; na
tazama, malaika akamgusa, akamwambia, Inuka, ule. 6 Akatazama, kumbe!
Pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake.
Akala, akanywa, akajinyosha tena. 7 Malaika wa Bwana akamwendea mara ya
pili, akamgusa, akasema, Inuka, ule; maana safari hii ni kubwa mno
kwako. 8 Akainuka, akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho
siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu.
Kumbe unaweza ukapewa chakula cha kishetani ukatembea kwenye balaa kwa
chakula hicho mpaka ukaingia mautini na unatakiwa uangalie pale
unapokaribishwa chakula kunauzima humo. Lazima ujue mitego ya mwindaji
kwingine umefanikiwa lakini anaweza kukukamata kwenye chakula na
unatakiwa useme “Baba Mungu ninaweka Baraka kwenye chakula hiki kwa jina
la Yesu”.
Kunaweza kuwa na mauti na mauti sio tukio mauti ni roho ni jini kumbuka
wana wa manabii waliona roho ya mauti kwenye sufuria. Mtu anaweza
akanuizia jambo Fulani kwenye chakula. Kama Mungu alivyo na watu wake na
shetani naye ana watumishi wake. Wakiona imeshindikana kukuletea
chakula wanaanza kukuletea ndotoni, ndiomaana unakuta mtu anatafuna
akiwa amelala. Tulipookolewa tunalindwa na Mungu kwa njia ya Imani na
ndio maana unapotaka kulala lazima uombe na sio useme Bwana Yesu shuka
utulinde hapa! Tunaotenda kazi ni sisi tena kwa ujasiri unawaamuru
malaika wakulinde.
“Kwa jina la Yesu ikiwa tatizo langu lilianza kwenye chakula nilichopewa
kuanzia leo ninakataa kwa jina la Yesu” ndoto ni bayana hakuna aliyeota
hakikutokea kina Ebimeleki,yusufu utawala, farao njaa, nebkandneza,
askari wa jeshi la midiani kwa mikate iliyoanguka toka mbinguni, hakuna
aliyeota ndoto haikutokea. Kama uko imara ndotoni unaota umekaribishwa
lakini wewe huli maana yakee uko imara. Wanaolishwa chakula ndotoni kama
uko juu unashushwa chini, kama unakazi unaipoteza kazi hiyo, kushindwa
kuomba.
Kunawatu wengi wamelishwa chakula nyumbani kwa mtu na wameharibikiwa
maisha yao ”kwa jina la Yesu kuanzia leo magonjwa niliyoyapata kwa
kulishwa chakula ndoton ninayakataa kwa jina la Yesu mahala popote
nilipokula chakula cha kichawi kuanzia leo enyi mashetani mlioniwekea
kutokuolewa kutokufanikiwa kuanzia leo ninawafyeka kwa jina la Yesu
navunja maagano yaliyokuwa ndani ya chakula ninayavunja kwa jina la Yesu
maagano ya mauti, maagano ya kifo ninayavunja kwa jina Yesu ninaagiza
kuanzia sasa majini, majoka , mizimu walionuiziwa kwenyee chakula cha
ndotoni, kwenye chakula cha mwilini kuazia leo ninakataaa kwa jina la
Yesu”.( ukitaka kutatua tatizo unatakiwa ujue chanzo cha tatizo”)
Wengine kwa njia ya chakula wanaweza kuchukua nyota yako wananuizia
kabisa na hakuna kinachotokea chenyewe vitu vinatengenezwa ndio maana
duniani
Kuna watu wa aina tatu.
1. Wale wanaoona matukio yanatokea tu lakini hawajuwi
kinachoendelea.
2. Wale wanaojua kinachoendelea; wakiona nchi wanajua
kinachoendelea wakiona mtu kafa wanajua kinachoendelea
3. Watu wanaotengeneza mambo yatokee wakitaka upatwe ugonjwa
unapatwa na ugonjwa.
Tukidili na chanzo cha tatizo tunalimaliza tatizo, kuna mamlaka ya
rohoni inayotegemewa kusimamisha mambo Fulani. Maisha ya mtu hujulikana
kabla hayajaanza; Yeremia anasema Kabla sijakuumba katika tumbo
nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa
nabii wa mataifa. Inawezekana wamekupotezea miaka mingi lakini Mungu
anaweza kukurudishia vyote vilivyopotea, Mungu ni Mungu wa nafasi ya
pili na usiangalie vile ulivyo Biblia inasema amelaaniwa yeye
amtegemeaye mwanadamu kwa jambo lolote.
Baraka ndani ya chakula na laana ndani ya chakula, kabla hujazaliwa
Baraka zako zinaonekana ukiwa tumboni mwa mama yako. Kuna wakati
mwingine mtu huwa hapendi lakini hubalansi kwasababu ya urafiki, kuna
mambo unakula leo halafu madhara yanaanza mwaka kesho. Haung’ai
kwasababu unavyoonekana kwa nje hapana bali kuna kitu kimewekwa ndani
yako na Mungu na wachawi hukiona na kukichukua na wewe unadhani
unafanyiwa fitina kumbe ulipewa chakula kilichonuiziwa.
Kilichowekwa ndani yako kinakupigisha hatua kwa elimu na kisipokuwepo
unakuta unasoma lakini hauwezi kufanikiwa kumbe ni chakula. “Kwa jina la
Yesu ninajikinga na chakula au vinywaji au kitu chochotee kilichotolewa
sadaka kwa mashetani na mtu yeyote aliyetoa sadaka ninamteketeza kwa
jina la Yesu chochote alichonipa mtu ndugu rafiki au mtu yeyote bila
kujua nikala au nikanywa kuanzia leo yamrudie yeye mwenyewe kwa jina la
Yesu” unamatatizo na haujui matatizo hayo yanatokea wapi na kuwa wa
kwanza darasani sio kuwa na maisha mazuri lakini Mungu ameweka kitu
ndani ya mtu nyota uwezo karama imewekwa ndani ya mtu na elimu
inamsaidia mtu huyo. Kila chakula unachokula lazima kiwe kimetolewa
sadaka mahali Fulani na ndio maana watu wa Mungu wanapotaka kula
wanakiombea “kwa jina la Yesu ninawashinda wote walioandaa chakula wiki
hii kwenye ndoto, kwenye sherehe nawashinda kwa jina la Yesu”
Unapokaribishwa chakula lazima uangalie unaweza kula kilichonuiziwa na
shida watu wamezoea kuombewa, unatakiwa ujifunze kupigana wewe mwenyewe
unapiganaje unapigana kwa jina la Yesu”kwa jina la Yesu kila chakula
kilichoandaliwa kichukue nyota naamuru roho yangu ikatae kwa jina la
Yesu. Kwa jina la Yesu kila aliyeandaa chakula cha mauti, kinywaji cha
kifo namrudishia yeyee kwa jina la Yesu aliye andaa kwenye ndoto au
mahala popote ninakataa kwa jina la Yesu” kila unachosema kinakuwa.
Kwanini ninasisitiza kuomba mathayo10: 8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu,
takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure. Kila mtu
aliyempokea Yesu anauwezo 1 Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili,
akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na
udhaifu wa kila aina. Marko7:6 luka 10:19 Tazama, nimewapa amri ya
kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu
kitakachowadhuru. Kwahiyo usiseme niombeeni unatakiwa uvunje mwenyewe
kama unamjua mchawi unamtaja na jina Mathayo18: 18 Amin, nawaambieni, yo
yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote
mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni. Vita vya rohoni
ni kwamba wewe unaomba ukitaja maneno na utakuwa vile unavyoamini. Sisi
mbele za Mungu ni watoto wa Mungu na Mungu hutenda sawa na vile vile
unavyoamini, ukiamini nikimfunga shetani anafungika na inakuwa hivyo
hivyo ulivyoamini.
III. UKIRI
Baba wa mbinguni nimeisikia sauti yako na ninaomba nguvu ya uweza
kushindana na wakala wote wa shetani na kila mtu aliye nihusisha kwa
jambo lolote la kuweza kunisababishia uharibifu ndani yangu leo
ninaomba asipate nguvu juu yangu na kwasababu hiyo ninapokea nguvu na
kujitakasa.
IV. MAOMBI
Katika jina la Yesu kristo mwana wa Mungu aliye hai ninavunja mashetani
yote yaliyoingizwa kwenye familia yangu kwa njia ya chakula kwa jina
la Yesu. Ninasambaratisha kuanzia sasa magonjwa yaliyopandwa kwa njia ya
chakula ninayaharibu na kuyaangamiza kwa jina la Yesu, kila kufeli,
kuanguka kulikosababishwa kwa njia ya chakula ninasimama kinyume nacho
kwa damu ya mwana Kondoo, kila kinywaji nilichokinywa kila kushindwa
kulikosababishwa kwasababu ya chakula ninasambaratisha kwa jina Yesu,
ninaharibu wasimamizi wa chakula mlioungamanishwa na chakula kwa damu ya
mwanakondoo, ninafungua vingufungo vyote vilivyofungwa na wakala wa
shetani kwenyee familia yangu na maisha yangu kwa njia ya chakula
ninabomoa kwa damu ya mwanakondo katika jina la Yesu, mauti iliyoingia
kwa njia ya chakula ninaiharibu kwa jinala laYesu, ninaharibu udhaifu
wowote ulionuiziwa kwenye chakula juu yangu kwa damu ya mwana kondoo,
“vita sio vyangu vita ni vya Bwana” ninaharibu kila chanzo cha magonjwa,
mikosi, kukataliwa, ninafungua kamba zote katika jina la Yesu. Kwa jina
la Yesu kila atakaye niletea zawadi au chakula kwa njia ya siri
naiamuru laana ile imrudie yeye kwa jina la Yesu lakini mimi sitalogwa
kwa jina la Yesu.
AMEN.
Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
No comments:
Post a Comment