Ufufuo na Uzima Kawe. Neno mchawi
limeandikwa mara nane kwenye Biblia tena kwa mkazo; neno wachawi limeandikwa
mara ishirini, uchawi mara kumi na nne, uganga mara kumi na nane, waganga mara
ishirini na moja na mapepo mara mia moja na arobaini na moja. Ni muhimu na
lazima mambo haya yahubiriwe ili watu waweze kuyaelewa na waweze kuwa huru.
“Tena mtu mume au mtu mke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa;
watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao.” Walawi 20:27 Maana ya Laana
Laana ni zaidi ya kuwa mgonjwa. Ni pale ambapo maisha ya mtu yanakosa muelekeo;
kila unalolianza hulimalizi, ikiwa asubuhi unatamani iwe mchana na mchana
unatamani iwe usiku. Ukiwa huna watoto unawatamani ukiwapata unatamani
usingekuwa nao. Hayo ndio maisha ya laana. Yaliyojaa misukosuko, kukosa amani
na furaha kutoweka kabisa. Laana inaweza kumpata mtu kutoka kwa mchawi au
mshirikina ambaye anakuwa na wivu juu ya maisha yako. Ni vizuri ujue kuwa
katika kila familia lazima kunakuwa na mtu mshirikina au mchawi. Na siku zote
kamba za kufungwa na mtu anayekujua zinatenda kazi vizuri kuliko kamba za mtu
asiyekujua. Lakini laana pia yaweza kumpata mtu anapoacha kuisikiliza sauti ya
Mungu. Biblia inaeleza kwa kirefu namna maisha ya mtu mwenye laana yalivyo.
“Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie
kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo
zitakapokujia laana hizi zote na kukupata. Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na
mashambani. Litalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia. Utalaaniwa uzao
wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa
kondoo zako. Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo, Bwana atakuletea laana
na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata
uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo.
Bwana atakuambatanisha na tauni, hata atakapokwisha kukuondoa katika nchi
uingiayo kwa kuimiliki. Bwana atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa,
na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo
vitakufukuza hata uangamie. Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa
shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma. Bwana atafanya mvua ya nchi yako
iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni hata uangamie. Bwana
atakufanya upigwe mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini
utakimbia mbele yao kwa njia saba; nawe utatupwa huko na huko katika falme zote
za duniani. Na mzoga wako utakuwa chakula cha ndege wote wa angani, na wanyama
wote wa duniani, pasiwe na mtu wa kuwafukuza. Bwana atakupiga kwa majipu ya
Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa.
Bwana atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni; utakwenda
kwa kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi
katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na
mtu wa kukuokoa. Utaposa mke na mume mwingine atalala naye; utajenga nyumba
usiikae; utapanda mizabibu usitumie matunda yake. Ng'ombe wako atachinjwa mbele
ya macho yako, usile nyama yake; utanyang'anywa punda wako mbele ya uso wako
kwa jeuri, usirudishiwe; kondoo zako watapewa adui zako, usipate mtu wa
kukuokoa. Wanao na binti zako litapewa taifa lingine, na macho yako
yataangalia, na kuzimia kwa kuwatamani mchana kutwa; wala hapatakuwa na kitu
katika uwezo wa mkono wako. Matunda ya nchi yako, na taabu yako yote, vitaliwa
na taifa usilolijua; utaonewa tu, na kupondwa chini daima; hata uwe mwenye
wazimu kwa yaonwayo na macho yako, utakayoyaona. Bwana atakupiga magoti na
miguu kwa jipu lililo zito, usilopata kupozwa, tokea wayo wa mguu mpaka utosi
wa kichwa. Bwana atakupeleka wewe, na mfalme wako utakayemweka juu yako, kwa
taifa usilolijua wewe wala baba zako; nawe huko utatumikia miungu mingine ya
miti na mawe. Nawe utakuwa ushangao, na mithali, na dharau, kati ya mataifa
yote huko atakakokuongoza Bwana. Mbegu nyingi utazichukua nje shambani, lakini
utavuna haba, kwa kuwa nzige watazila. Utapanda mizabibu na kuitengeza, wala
hutakunywa katika divai yake, wala kuichuma kwani italiwa na mabuu. Utakuwa na
mizeituni katika mipaka yako yote usijipake mafuta yake; kwa kuwa mzeituni wako
utapukutika. Utazaa wana na binti, lakini hawatakuwa wako wewe; kwa sababu
watakwenda utumwani. Miti yako yote, na mazao ya nchi yako, nzige watakuwa
nayo. Mgeni aliye kati yako atazidi kupaa juu yako; nawe utazidi kushuka chini.
Yeye atakukopesha, wala wewe usimkopeshe; yeye atakuwa ni kichwa, wewe utakuwa
mkia. Na laana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na kukupata, hata
uangamizwe, kwa kuwa hukuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, kushika maagizo
yake na amri zake alizokuagiza; nazo zitakuwa juu yako kwa ishara na ajabu, na
juu ya uzao wako milele; kwa kuwa hukumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa furaha na
moyo wa kushukuru, kwa ajili ya ule wingi wa vitu vyote; kwa hiyo utawatumikia
adui zako atakaowaleta Bwana juu yako, kwa njaa, na kwa kiu, na kwa uchi, na
kwa uhitaji wa vitu vyote; naye atakuvika kongwa la chuma shingoni mwako, hata
atakapokwisha kukuangamiza. Bwana atakuletea taifa juu yako kutoka mbali,
kutoka ncha ya dunia, kama arukavyo tai; taifa usilolifahamu ulimi wake; taifa
lenye uso mkali, ambalo haliangalii uso wa mzee, wala halipendelei kijana; naye
atakula uzao wa ng'ombe wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako mpaka
utakapokwisha kuangamizwa; wala hatakuachia nafaka, wala divai, wala mafuta,
wala maongeo ya ng'ombe wako, wala wana-kondoo wako, hata atakapokwisha
kukuangamiza. Naye atakuhusuru katika malango yako yote, hata kuta zako ndefu,
zenye maboma, ulizokuwa ukiziamini, zishuke, katika nchi yako yote kila upande;
naye atakuhusuru katika malango yako yote kila upande, katika nchi yako yote
aliyokupa Bwana, Mungu wako. Nawe utakula uzao wa tumbo lako mwenyewe, nyama ya
wana wako na binti zako aliokupa Bwana, Mungu wako; katika mazingirwa na katika
mkazo utakaokazwa na adui zako. Mtu mume kati yenu aliye mwororo na laini sana,
jicho lake litakuwa ovu juu ya nduguye, na juu ya mke wa kifuani mwake, na juu
ya masalio ya wanawe waliosalia naye; hata asitake wao mmojawapo apewe katika
nyama ya wanawe atakaowala, kwa kuwa hana kitu kilichomsalia kwake; katika
mazingirwa na mkazo utakaokazwa na adui yako katika malango yako yote. Mwanamke
kati yenu aliye mwororo na laini, ambaye hangehatirisha kuweka wayo wa mguu
wake nchi kwa umalidadi na ulaini, jicho lake huyu litakuwa ovu juu ya mume wa
kifuani mwake, na juu ya mwanawe, na juu ya binti yake, na juu ya mchanga wake
atokaye katikati ya miguu yake, na juu ya wanawe atakaowazaa; kwa kuwa atawala
kwa siri, kwa uhitaji wa vitu vyote; katika mazingirwa na mkazo utakaokazwa na
adui yako katika malango yako. Kama hutaki kutunza kufanya maneno yote ya
torati hii yaliyoandikwa katika kitabu hiki, upate kulicha jina hili la fahari
na utisho, Bwana Mungu wako; ndipo atakapofanya Bwana mapigo yako yawe ya
ajabu, na mapigo ya uzao wako, mapigo makubwa kwa kweli, ya kudumu sana, na
magonjwa mazito ya kudumu sana. Naye atakurejezea maradhi yote ya Misri juu
yako uliyokuwa ukiyaogopa, nayo yataambatana nawe. Tena kila ugonjwa, na kila
pigo yasiyoandikwa katika kitabu cha torati hii, atakutia nayo Bwana juu yako,
hata utakapokwisha kuangamizwa. Nanyi mtasalia wachache kwa hesabu, ninyi
mliokuwa mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi; kwa kuwa hukuisikiza sauti ya
Bwana, Mungu wako. Tena itakuwa, kama vile alivyokuwa akifurahi Bwana juu yenu
kwa kuwatendea mema na kuwafanya kuwa wengi, ndivyo atakavyofurahi Bwana juu
yenu kwa kuwapoteza na kuwaangamiza; nanyi mtanyakuliwa katika hiyo nchi
mwingiayo kuimiliki. Bwana atakutawanya katika mataifa yote, tokea ncha hii ya
dunia hata ncha hii ya dunia; nawe huko utatumikia miungu mingine usiyoijua
wewe wala baba zako, nayo ni miti na mawe. Wala katika mataifa hayo hutapata
raha iwayo yote, wala hutakuwa na kituo cha wayo wa mguu wako; lakini Bwana
atakupa huko moyo wa kutetema, na macho ya kuzimia, na roho ya kudhoofika; na
uzima wako utakuwa na wasiwasi mbele yako; nawe utakuwa na woga usiku na
mchana, wala hutaamini kamwe maisha yako; asubuhi utasema, Laiti ingekuwa
jioni! Na jioni utasema, Laiti ingekuwa asubuhi! Kwa kicho cha moyo wako
utakavyokucha, na kuona kwa macho yako utakavyoona.” Kumbukumbu 28: 15-67
Unakuta unazaa watoto hata uwafundishe vipi hawaelewi, umekuwa mtu wa mashaka na
kuonewa, kila ukianza biashara unakuwa unaishia na madeni na kufilisika. Chanzo
ni laana hiyo, tauni inayoongelewa kwenye biblia ni magonjwa kama kifua,
mgongo, homa zinakuwa haziishi, bumbuazi la moyoi unakuwa umeeduwaa tu; unaposa
mchumba lakini mwingine anakuja kumwoa, unaanza mradi haufanikiwi, ngombe wako
anachinjwa mbele ya macho yako maana yake unapigwa roba au kabari na kuibiwa
huku unajiona, Shida hizi zinaweza kuwa zinakupata na hujui kwa nini au nini
chanzo chake. Chanzo cha yote haya chaweza kuwa ni laana ya wachawi. Laana ya
Kichawi “Kisha wana wa Israeli wakasafiri na kupanga katika nchi tambarare za
Moabu ng'ambo ya pili ya Yordani karibu ya Yeriko. Na Balaki mwana wa Sipori
akaona mambo yote ambayo Israeli wamewatendea Waamori. Moabu akawaogopa hao
watu sana, kwa kuwa walikuwa wengi; Moabu akafadhaika kwa sababu ya wana wa
Israeli. Moabu akawaambia wazee wa Midiani, Sasa jeshi hili la watu litaramba
vitu vyote vinavyotuzunguka, kama vile ng'ombe arambavyo majani ya mashamba. Na
Balaki, mwana wa Sipori, alikuwa mfalme wa Moabu zamani zile. Basi akatuma
wajumbe kwa Balaamu mwana wa Beori, hata Pethori, ulio kando ya Mto, mpaka nchi
ya wana wa watu wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna watu waliotoka
Misri; tazama, wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili mimi. Basi,
njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi.
Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa
maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa.
Wazee wa Moabu, na wazee wa Midiani, wakaenda, wakichukua ujira wa uganga
mikononi mwao; wakamfikilia Balaamu, wakamwambia maneno ya Balaki. Akawaambia,
Kaeni hapa usiku huu, nami nitawaletea jawabu kama Bwana atakavyoniambia; wakuu
wa Moabu wakakaa na Balaamu. Mungu akamjia Balaamu, akasema, Ni watu gani hawa
ulio nao pamoja nawe? Balaamu akamwambia Mungu, Balaki mwana wa Sipori, mfalme
wa Moabu, amewatuma kwangu, akisema, Tazama, kuna watu waliotoka Misri,
wanaufunika uso wa nchi; basi njoo unilaanie watu hawa; labda nitaweza kupigana
nao, na kuwafukuza.” Hesabu 22:1-11 Kumbe unaweza kuwa una nguvu ya kumshinda
mtu lakini unapolaaniwa unakuwa hauna kitu tena. Unaweza kuwa una elimu lakini
ukilaaniwa elimu yako haiwezi kukusaidia kuishi maisha mazuri. Wana wa Israeli
walisafiri jangwani wakapata njaa Mungu akawapa mana kutoka mbinguni na mavazi
yao hayakuchakaa kwa muda wa mika arobaini , wakapata kiu mwamba ukatoa maji
jangwani, wakaugua naye yule nyoka wa moto akawatokea wakaponywa. Walipofika kwenye
bahari ya Shamu, ikagawnyika wakavuka huku farasi na wapanda farasi wa majeshi
ya Farao akatupwa baharini. Balaki mwana wa Moabu alipoona wana wa Israeli
wanaelekea kwenye nchi yao ya ahadi akamkodisha mchawi aje kuwalaani. Hata wewe
leo wapo kina Balaki wa maisha yako ambao wameona umepita vikwazo na magumu
mengi na sasa unakaribia kulifikia lile kusudi la Mungu katika maisha yako;
wameazimia kuona unaharibikiwa hivyo wanakulaani kama wachawi au kama sio
wanakodisha mchawi akulaani kwa niaba yao kama Balaki alivyomtumia Balamu
kuwalaani wana wa Israeli.. Kwenye ulimwengu wa rohoni kuna viashiria
vinavyoonyesha mtu atakuwaje siku zijazo na watu ambao hawakupendi wanapoona
unaelekea kwenye mafanikio wanamkodisha mtu mchawi ili akulaani. Lakini sisi
tuliookolewa kwa damu ya mwanakondoo Yesu Kristo tuna nguvu ya kuwashinda wao
maana wao wanategemea hirizi, na kafara zao lakini sisi tunamtegemea Bwana wa
majeshi. Laana inapotumwa huruka na kwenda kuingia sehemu husika na inajua
ingie kwa nani na isingie kwa nani. “Balaamu akamwambia Balaki, Nijengee hapa
madhabahu saba, ukaniandalie hapa ng'ombe waume saba, na kondoo waume saba.
Balaki akafanya kama Balaamu alivyonena. Balaki na Balaamu wakatoa sadaka,
ng'ombe mume mmoja na kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu. Balaamu
akamwambia Balaki, Simama karibu na sadaka yako, nami nitakwenda, labda Bwana
atakuja kuonana nami; na lo lote atakalonionyesha nitakuambia. Akaenda hata
mahali peupe juu ya kilima. Mungu akakutana na Balaamu; naye Balaamu
akamwambia, Nimetengeneza madhabahu saba, nami nimetoa sadaka ng'ombe mume
mmoja na kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu. Bwana akatia neno katika
kinywa chake Balaamu, akasema, Umrudie Balaki; ukaseme maneno haya. Akarudi
kwake, na tazama, amesimama karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, yeye na wakuu
wote wa Moabu pamoja naye. Akatunga mithali yake, akasema, Balaki amenileta
kutoka Aramu, Mfalme wa Moabu kutoka milima ya mashariki, Njoo! Unilaanie
Yakobo, Njoo! Unishutumie Israeli. Nimlaanije, yeye ambaye Mungu hakumlaani?
Nimshutumuje, yeye ambaye Bwana hakumshutumu?” Hesabu 23: 1- 8 Mchawi Balaam
alitataka madhabahu saba ili awalaani wana wa Israeli siku saba za wiki. Laana
ya mchawi haina jumapili wala jumatatu bali ni siku zote. Pia tumeona amewatoa
kondoo na ngombe kama kafara juu ya kila madhabahu. Katika wanyama watolewao
kafara juu ya madhabahu ng’ombe ndiye mkubwa kuliko wote na kondoo mdogo kuliko
wote. Hii inamaanisha kuwa kwenye mambo makubwa wanakulaani na kwenye mambo
madogo pia. Kwa hiyo yule mtu ambaye hakupendi anamwendea mchawi halafu
wanaandaa madhabahu na kuchinja mnyama ili damu ambayo ni uhai imwagike kwenye
madhabahu. Mashetani huja kwenye ile madhabahu na kunywa ile damu inayomwagika
na baadaye huelekezwa kwako ili waje kukuwekea hiyo laana. “lakini, kama
ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala
hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia
wampendao. Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote,
hata mafumbo ya Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu
ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna
ayafahamuye ila Roho wa Mungu.” 1 Wakorintho 2:9-11 Yapo mambo makubwa ambayo
Mungu ameandaa kwa ajili ya maisha yako. Pale ulipo leo si kitu kabisa ipo
sehemu njema unayoelekea kesho. Mahali ambapo hutatikisika tena na utasahau
taabu yako. Wewe ambaye ni mbilikimo leo kesho utakuwa baunsa. Mungu tunaye
mtumikia ni Mungu anayejua tutokako na tuendako. Ukikubali kumsikiliza Mungu
hakika atasema na Balaam wa maisha yako kama alivyosema kipindi kile cha wana
wa Israeli; kwamba “huweezi kumlaani aliyebarikiwa.” Kama Mungu ndiye
aliyekubariki sio mchawi wala mshirikina atakayeweza kukulaani. Lakini uwe na
baraka kutoka kwa Mungu ambayo hupatikana kwa kuisikiliza sauti yake.
Utakapolaaniwa na Mungu pia, hakuna atakayekubariki ukabarikiwa. Balaam Alikuwa
ni Mchawi si Nabii wa Bwana. Kwa nini mchawi huyu Balaam anasikia sauti ya
Bwana kama sio nabii wa Bwana? Ni kwa sababu mtu anapoingia kwenye ulimwengu wa
rohoni anakuwa anawaona wote Mungu na malaika zake pamoja na shetani na mapepo
yake. Hivyo Mungu aliingilia mawasiliano ya Balaam na shetani na kumpa
maelekezo yake kwa kuwa alikuwa anawalinda wana wa Israeli. Balaam yeye atakuwa
alidhani kuwa Mungu ni ngazi fulani ya juu katika utawala wa shetani ambao yeye
hajafikia. Baadaye huyu mchawi Balaam alikuja kufia mikononi mwa wana wa
Israeli. “Balaamu naye, huyo mwana wa Beori, huyo mchawi, wana wa Israeli
walimwua kwa upanga kati ya hao wengine waliowaua.” Yoshua 13:22 Madhabahu za
Laana za Kichawi. Wachawi hawawezi kuloga bila madhabahu. Ili waweze kuyatuma
mashetani yafanyike laana kwenye maisha yako ni lazima madhabahu ijenge kwanza.
Kisha lazima kafara itolewe juu ya madhabahu hiyo ili ule uhai ambao umo katika
damu uyahuishe yale mashetani ambayo hufanyika laana. Pasipo hiyo madhabahu
laana haiwezi kufanyika kwako. Hivyo ni muhimu kuzishughulikia madhabahu
zilizoinuliwa ili wewe ulaanike. Zinapobomoka zile, wewe unarudi kwenye kusudi
la Mungu juu ya maisha yako. UKIRI: Ninazivunja laana za wachawi na waganga wa
kienyeji kwa damu ya mwaanakondoo. Madhabahu saba zenye kafara saba zilizo juu
yangu ninazivunja kwa damu ya Yesu. Kuanzia leo kila madhabahu ya kuzimu ya
Lucifer, nabii wa uongo ninaifyeka kwa damu ya Yesu, maaskari wa kishetani
ninawafyeka na madhabahu zao kwa jina la Yesu Kristo. Ninasimama kinyume na
kuzimu, ninateketeza nia ya kuzimu kwa jina la Yesu. Imeandikwa; “laana isiyo
na sababu haimpati mtu” Ninaibomoa madhabahu ya kila laana iliyo juu ya maisha
yangu kwa jina la Yesu. Kwa jina la Yesu ninabomoa madhabahu za laana za
kichawi. Madhabahu za kushindwa, madhabahu za kuzimu zilizojengwa juu yangu,
madhabahu za laana ya ukoo wangu; ninazivunja kwa jina la Yesu! Ninavaa silaha
za vita, ninawafyeka wasimamizi wote wa laana za kichawi kwa jina la Yesu,
ninawateketeza kwa damu ya mwanakondoo. Ewe laana uliy kwenye maisha yangu
ninakufuta kwa jina la Yesu, ninateketeza laana za kishetani zilizotumwa kwangu
na familia yangu kwa damu ya Yesu. Ninazivunja laana zote za kishetani
zilizotumwa kwangu kwa jina la Yesu. Ewe laana ya nchi uliyoishikilia nchi
yangu ninakuamuru achia nchi yangu kwa jina la Yesu. Madhabahu za laana ya
kushindwa, laana ya kukataliwa, laana ya kukosa mke/mume; ninaibomoa kwa jina
la Yesu. Ninazibomoa madhabahu zote za kichawi kwa jina la Yesu. Madhabahu za
laana juu ya familia yangu ninazivunja kwa damu ya mwanakondoo. Kwa jina la
Yesu ninavunja laana juu ya ndoa yangu kwa, ninavunja laana juu ya masomo
yangu, ninazivunja madhabahu za kishetani zilizoshikilia laana juu ya biashara
yangu kwa jina la Yesu. Kwa damu ya mwanakondoo, maneno ya laana yaliyotamka na
wanadamu juu yangu na familia yangu ninayavunja kwa jina la Yesu. Imeandikwa;
“ni nani asemaye neno ikiwa Bwana hakuliagiza likatendeka?” Hii laana
haijaagizwa na Bwana, ninaibatilisha kwa damu ya mwanakondoo. Ninawateketeza
majini na mashetani wote mlioshikilia laana juu ya nchi na familia yangu kwa
jina la Yesu. Ninavunja laana za majeshi ya pepo wabaya kwenye maisha yangu kwa
jina la Yesu. Ninavunja madhabahu za wachawi zilizomwagiwa damu ya kafara
inenayo laana juu ya maisha yangu; ninazivunja kwa damu ya mwanakondoo, katika
jina la Yesu Kristo. AMEN!
No comments:
Post a Comment