Monday, December 21, 2015
KIAPO CHA KICHAWI Na Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima.
Mambo
ya Walawi 5:4- “Au, kama mtu akijiapisha, kwa kutamka haraka kwa midomo yake,
kutenda uovu, au kutenda mema, neno lo lote mtu atakalolitamka kwa kiapo pasipo
kufikiri, na neno hilo likamfichamania; hapo atakapolijua, ndipo atakapokuwa na
hatia katika mambo hayo mojawapo” Kuapa kunaweza kuwa kuapa kwa kutenda uovu au
kutenda jambo jema. Biblia inaongozwa kwa kiapo cha Mungu kwa wanadamu kuna
mambo mengine Mungu anawafanyia watu kwasababu aliwaapia watu hivyo hawezi
kuacha kutokuyafanya. Kwenye nguvu ya kiapo mtu unaweza kuapa jambo zuri ili
ulifanye. Wana wa Israeli walipokuwa wanaodoka Misri walifika katika mto Yordan
Yoshua 9:1- “Kisha ikawa hapo wafalme wote waliokaa ng'ambo ya pili ya Yordani,
hapo penye nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika upande wa pwani yote ya
bahari kubwa kuikabili Lebanoni, yaani, huyo Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na
Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, waliposikia habari ya mambo hayo; ndipo
walipojikutanisha pamoja wenyewe kwa wenyewe, ili kupigana na Yoshua, na hao
Israeli, kwa nia moja. Lakini wenyeji wa Gibeoni waliposikia habari ya hayo
yote Yoshua aliyokuwa amewatenda watu wa Yeriko, na wa Ai, wao wakatenda kwa
hila, nao wakaenda na kujifanya kama ndio wajumbe, wakaenda na magunia makuukuu
juu ya punda zao, na viriba vya mvinyo vilivyokuwa vikuukuu vilivyoraruka-raruka,
na kutiwa viraka; na viatu vilivyotoboka na kushonwa-shonwa katika miguu yao,
na mavao makuukuu waliyokuwa wanavaa; tena mkate wote wa chakula chao ulikuwa
umekauka na kuingia koga. Nao wakamwendea Yoshua hata maragoni huko Gilgali,
nao wakamwambia yeye na watu wa Israeli, Sisi tumetoka nchi ya mbali sana; basi
kwa hiyo fanyeni agano pamoja nasi. Basi watu wa Israeli wakawaambia hao
Wahivi, Labda mwakaa kati yetu; nasi tutawezaje kufanya agano nanyi? Nao
wakamwambia Yoshua, Sisi tu watumishi wako. Yoshua akawauliza, Ninyi ni nani?
Nanyi mwatoka wapi? Nao wakamwambia, Sisi watumishi wako twatoka nchi iliyo
mbali sana, kwa sababu ya jina la Bwana, Mungu wako; kwa kuwa sisi tumesikia
sifa zake, na habari ya hayo yote aliyofanya huko Misri, na habari ya hayo yote
aliyowatenda wale wafalme wawili wa Waamori, waliokuwa huko ng'ambo ya pili ya
Yordani, maana huyo Sihoni, mfalme wa Heshboni, na Ogu, mfalme wa Bashani,
aliyekuwa huko Ashtarothi. Kisha wazee wetu, na wenyeji wote wa nchi yetu,
walinena nasi na kutuambia, Chukueni vyakula mkononi mwenu kwa ajili ya safari,
mwende mkawalaki watu hao, na kuwaambia, Sisi tu watumishi wenu; basi sasa
fanyeni agano nasi. Huu mkate wetu tuliutwaa ukali moto katika nyumba zetu,
siku hiyo tuliyotoka kuja kwenu, uwe chakula chetu; lakini sasa, tazama,
umekauka, na kuingia koga; na viriba vyetu hivi, tulivyovitia divai, vilikuwa
ni vipya; sasa, tazama, vimeraruka-raruka; na haya mavazi yetu na viatu vyetu
vimekuwa vikuukuu kwa vile tulivyokuja safari ya mbali sana. Basi hao watu
wakatwaa katika vyakula vyao, wala wasitake shauri kinywani mwa Bwana. Naye
Yoshua akafanya amani pamoja nao, na kufanya agano nao, ili kwamba waachwe hai;
na wakuu wa mkutano wakawaapia. Kisha ikawa, mwisho wa siku ya tatu baada ya
kufanya hilo agano nao, walisikia habari ya kuwa watu hao ni jirani zao, na ya
kwamba waliketi kati yao. Kisha wana wa Israeli walisafiri, wakaifikilia miji
ya watu hao siku ya tatu. Basi miji ya watu hao ilikuwa ni hii, Gibeoni, na
Kefira, na Beerothi, na Kiriath-yearimu. Wana wa Israeli hawakuwapiga, kwa
sababu wakuu wa mkutano walikuwa wamekwisha kuwaapia kwa Bwana, Mungu wa
Israeli. Nao mkutano wote wakawanung'unikia hao wakuu. Lakini wakuu wote
waliwaambia mkutano wote, Sisi tumewaapia kwa Bwana, Mungu wa Israeli; basi
sasa hatuwezi kuwagusa watu hawa. Tutawafanyia neno hili, kisha tutawaacha wawe
hai; hasira isije juu yetu, kwa ajili ya hicho kiapo tulichowaapia. Wakuu
waliwaambia, Waacheni wawe hai; basi wakawa wenye kupasua kuni, na wenye kuteka
maji, kwa ajili ya mkutano wote; vile vile kama hao wakuu walivyowaambia. Basi
Yoshua akawaita, akanena nao, na kuwaambia, Mbona ninyi mmetudanganya, huku
mkisema, Sisi tu mbali sana na ninyi; nanyi kumbe! Mwakaa kati yetu? Basi sasa
mmelaaniwa kisha hatakosekana kuwapo mtu wa kwenu aliye mtumwa, wenye kupasua
kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu. Nao wakamjibu
Yoshua, na kusema, Ni kwa sababu ya sisi watumishi wako kuambiwa hakika, jinsi
huyo Bwana, Mungu wako alivyomwamuru mtumishi wake Musa kuwapa ninyi nchi hii
yote, na kuwaangamiza wenyeji wote wa nchi hii watoke mbele zenu; kwa sababu
hii tuliogopa mno kwa ajili ya uhai wetu kwa sababu yenu, nasi tumefanya neno
hili. Basi sasa, tazama, sisi tu mkononi mwako; basi kama uonavyo kuwa ni vyema
na haki kwako wewe kututenda, tutende vivyo. Naye akawafanyia hivyo, na
kuwaokoa na mkono wa wana wa Israeli, ili wasiwaue. Siku iyo hiyo Yoshua
akawafanya kuwa ni wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya
mkutano, na kwa ajili ya madhabahu ya Bwana, hata siku hii ya leo, katika
mahali hapo atakapopachagua.” Wana wa Israeli wametoka katika nchi ya Misri
kwenda katika nchi ya ahadi na walipovuka mto Yordani walijiliwa na watu
waliovaa magunia na viatu vilivyo tobokatoboka vya zamani sana wakawaambia wana
wa Israeli kwamba walivyoanza kuondoka mkate wao ulikuwa wamoto na viatu vyao
na nguo zao zilikuwa mpya sana lakini ilikuwa si kweli walijifanya wanamjua
Mungu wa Israeli amewatuma wana wa Israeli kuwauwa watu wote watakaokutana nao
ili wamiliki mahali pao. Wale watu waliwaendea wana wa Israeli ili wapate kiapo
kutoka kwao ili wasiuwawe. Mkutano wa Israeli ulikutana na wale watu mbele ya
safari yao na kushindwa kuwauwa kwasababu walikwisha waapia hivyo Yoshua
akawafanya kuwa wapasua kuni, wabeba maji na kufanya kazi za ndani kwa wana wa
Israeli na Mungu wao. Kuna wakati wana wa Israeli waliingia vitani wakaapa
kwamba hatakula mtu wala kunywa mpaka washinde vita. Walipoingia porini
wakakuta masega ya asali yanamwaga Asali lakini hakuna mtu hata mmoja aliyejaribu
kunyoosha mkono wake kushukua hiyo asali kwasababu ya nguvu ya ile asali. Mtoto
wa mfalme alikuwa hayupo wakati wa kiapo kile lakini yeye alikula. Kiapo
kinaweza kumfunga mtu akiona jambo zuri lakini asiliguse. Mtoto wa Mfalme
Yonathan alihukumiwa kuuwawa japo hakuwepo wakati kiapo kilivyokuwa kikitolewa.
1Samweli 14:26- “Na hapo watu walipokwisha kuingia mwituni, tazama, hiyo asali
ilikuwa ikidondoka; walakini hakuna mtu hata mmoja aliyetia mkono wake
kinywani; kwa sababu hao watu walikuwa wakikiogopa kile kiapo. Ila Yonathani
hakusikia, hapo babaye alipowaagiza watu kwa kiapo; basi yeye akainyosha ncha
ya fimbo iliyokuwa mkononi mwake, na kuichovya katika sega la asali, kisha
akatia mkono wake kinywani; na macho yake yakatiwa nuru.” Mathayo 5:33- “Tena
mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo
zako” Yakobo 5:12 “Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu
wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; bali ndiyo yenu na iwe ndiyo,
na siyo yenu iwe siyo, msije mkaangukia hukumu.” Kwenye agano la kale watu
walikuwa wanaapa na kuangukia katika matatizo. Yeremia 11:1- “Neno hili ndilo
lililomjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, kusema, Yasikieni maneno ya maagano haya;
ukaseme na watu wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; ukawaambie, Bwana, Mungu wa
Israeli, asema hivi, Na alaaniwe mtu asiyeyasikia maneno ya maagano haya,
niliyowaamuru baba zenu, siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri, katika
tanuru ya chuma, nikisema, Itiini sauti yangu, mkafanye sawasawa na yote
niwaagizayo ninyi; ndivyo mtakavyokuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu;
ili nipate kukitimiza kiapo nilichowaapia baba zenu, kuwapa nchi ijaayo maziwa
na asali, kama ilivyo leo hivi. Ndipo nikajibu, nikasema, Amina, Ee Bwana.”
Moja wapo ya Sababu ambayo Mungu aliwapa nchi ya ahadi wana wa Israeli ni
kwasababu aliwaapia baba zao japo walikuwa wakimuudhi njiani lakini aliwaongoza
mpaka wakaifikia. Ezekieli 16:59 “Maana Bwana MUNGU asema hivi; Nitakutenda
vile vile kama ulivyotenda, uliyekidharau kiapo kwa kulivunja agano." Kuna
wakati Mungu alimwambia Musa ajitenge na wana wa Israeli ili awauwe wote lakini
Musa alimkumbusha kiapo alichowaapia Baba zao na kuna wakati watu walikuwa
wakitenda maovu lakini aliwavumilia mpaka akawafikisha kwenye Nchi ya ahadi.
Isaya 45:23 “Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika
haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi
utaapa” Mwanzo 22:16 “Akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa
umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee” Zaburi 119:109
“Nimeapa nami nitaifikiliza, Kuzishika hukumu za haki yako.” Isaya 54:9 “Kwa
maana jambo hili limekuwa kama maji ya Nuhu kwangu; maana kama nilivyoapa ya
kwamba maji ya Nuhu hayatapita juu ya dunia tena, kadhalika nimeapa ya kwamba
sitakuonea hasira, wala kukukemea.” Yeremia 44:16 “Ndipo watu wote waliojua ya
kuwa wake zao waliwafukizia uvumba miungu mingine, na wanawake wote waliosimama
karibu, mkutano mkubwa, yaani, watu wote waliokaa katika nchi ya Misri, katika
Pathrosi, wakamjibu Yeremia, wakisema, Neno lile ulilotuambia kwa jina la
Bwana, sisi hatutakusikiliza. Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno
lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na
kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme
wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu;
maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona
mabaya. Lakini tulipoacha kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia
sadaka za kinywaji, tumepungukiwa na vitu vyote; na kuangamizwa kwa upanga, na
kwa njaa.” Shetani naye ni mungu wa dunia hii na yeye ana majeshi yake ambayo
ni mapepo majini, miungu n.k. Matendo ya mitume 23:12-14 “Kulipopambauka,
Wayahudi wakafanya mapatano, wakajifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala
hawatakunywa hata wamwue Paulo. Na hao walioapiana hivyo walipata zaidi ya watu
arobaini. Nao wakaenda kwa wakuu wa makuhani na wazee, wakasema, Tumejifunga
kwa kiapo tusionje kitu hata tumwue Paulo.” Hakuna uharibifu unaompata mtu bila
kikao cha uharibifu iwe ni kwenye kazi, ndoa, safari, biashara. Biblia inasema
makuhani walikaa kikao ili wamuuwe Paulo. Watu Zaidi ya arobaini wameapa
kwaajili ya kumwangamiza mtu mmoja. Shetani hajaumba kitu chochote hutumia kile
alichokiumba Mungu na kukitumia kwa maslahi yake binafsi. Wachawi wamejifunga
kwa kiapo ili mtu fulani asishinde, asiolewe, asisafiri, asifanikiwe kwenye
jambo Fulani japo dalili zote zinaonyesha mtu Fulani anakaribia kushinda lakini
kuna watu wamekaa na kuwaendea wazee kuwaambia wamekaa na hawata kula wala
kunywa mpaka ashindwe, biashara yake iharibike, asiolewe. Bwana naye ameapa na
kusema hatakuacha wala hatakupungukia kabisa, Mungu ameapa na kusema kwa kupiga
kwake sisi tumeponywa na Mabaya hayatatupata sisi wala tauni haitakaribia
hemani mwetu. Watu wengi wanaapa ili Fulani asijenge, asizae, asioe au asiolewe
na viapo hivi hufanywa wakati wa usiku au mchana na wengine huapa kwa maneno
raihisi tu kwamba “tuone kama utafanikiwa” wengine wanaapa bila kula au kunywa
mpaka viapo vyao vitokee, wengine wameapa kule kijijini kwamba kwenye nyumba
yenu hakuna atakayefanikiwa lakini sisi tunaye Mungu wa Yakobo ambaye ametoa
ahadi zake kwetu kwa kiapo na zitatimia kwa jina la Yesu. Matatizo yako hayapo
mjini au kwenye wizara fulani bali ipo kule kijijini kule wale wazee wa kule
wamewahi kuapa kwaajili ya ukoo wenu kwamba kwenye familia yenu asitoke mbunge
au waziri au mtu atakaye safari nje ya nchi au mtu atakayefika chuo kikuu, waliapa
kwenye njia panda au kwenye visima visivyokauka na ile tarehe yao roho
mtakatifu aliiona tunaifua na kukivunja kile kiapo kwa jina Yesu. Vita sio
vyetu vita ni vya Bwana na Mungu wa mbinguni ameapa kwa nafsi yake
hatamdanganya Yakobo atamwambia yaliyo kweli. Unapokuwa na Yesu hauzuiliki
Tumeona Yonathan alikula asali japo hakuwepo wakati wa kiapo. “Katika jina la
Yesu leo kwa jina la Bwana wa majeshi ninavunja kiapo cha ukoo familia ndoa
kazi biashara walicho hapa kwamba mimi sitafanikiwa ninavunja kiapo kwa jina la
Yesu ninasafiri kwenda kwenye kijiji nilipozaliwa ilipo familia yangu ninavunja
kiapo cha kila aliyeapa kwamba mimi sitafanikiwa ninakivunja kiapo hicho kwa
jina la Yesu’ “Kwa jina la Yesu ninakataa kuharibikiwa sawasawa na kikao chao
kwa jina la Yesu, kiapo cha wazee wa kijiji, kiapo cha wazazi, kiapo cha
wachawi ninakivunja kwa jina la Yesu” Mungu ametuonyesha mambo mengi
yanaendelea kwasababu ya viapo. Kuna mtu alimwendea Yesu ili amponye mgonjwa
wake lakini Yesu alimwambia nenda nitakuja lakini mtu yule alimwomba Yesu aseme
neno tu mgonjwa wake apone ndipo Yesu akamwambia apone sawasawa na Imani yake,
yule mtu aliporudi alimkuta ameshapona na alipouliza amepona muda gani
wakamwambia muda ambao Yesu alikuwa na naye. Maana yake Neno moja linaweza
kumponya mtu na akafunguka kabisa kutoka kwenye kiapo chake. Kuna baadhi ya
familia nyumba zina na watoto wenye mama tofauti yaani Baba anakuwa anawake
wengi na inatokea kwenye nyumba moja watoto wa nyumba ile wanafanikiwa sana
kuliko wengine. Kinachokuw kimetokea ni kwamba wanakuwa wamewafunga wenzao kwa
viapo mfano asipatikane mtu wa kuwaoa au kuolewa nao, asipatikane mtu wa kusoma
mpaka chuo kikuu au kusafiri. Viapo hivyo vyote vinaondoka kwa Damu ya
mwakondoo Yesu kristo. Mungu alimpa Ibrahimu ahadi alipokuwa ana umri wa miaka
sabini na mitano na ahadi yake ikatimia Sara akiwa na miaka 90. Usiwe na
wasiwasi kwamba ndoto yako haitatimia bali unatakiwa ujue kazi ndio kwanza
imeanza na ndoto yako itafanikiwa kwa jina ya Yesu. Mungu alikuwa ameshaapa
atawatoa wana wa Israeli na kuwapeleka kwenye nchi ya ahadi, Yesu aliapa
msalabani kwamba Imekwisha, Ufufuo na uzima
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment